MAJIRA NA NYAKATI

MAJIRA NA NYAKATI YA SIKU YA LEO.
Siku ya NNE.
Lango la 25.
Mwezi ABIBU.
Mwaka wa 6 wa UKAMILIFU NA UTIMILIFU WA ISAYA 2:2-4 NA ISAYA 60.
(29 October 2016)
WARAKA NA:19–Lango la 3 Thebeti,5 [15 July,2016]
MIAKA 1000 YA KUTAWALA NA KRISTO.
Makuhani Wote wa Njia
Makuhani  Wote wa Njia Watendaji
Makuhani wa Mikoa
Makuhani wa Vituo Vyote
Taifa la Gosheni (Tanzania) na Nje ya Gosheni

YAH:    UJUMBE MAALUM KWA KANISA LA MWISHO

Shika Neno Mliopewa Neema Kubwa,
Mtakumbuka baada ya Unyakuo wa Kristo Kizazi cha Nne, niliapa mara nyingi  nikiwa madhabahuni kuwa Kanisa la Siloam halitapasuka milele. Nilikuwa nafuta 1Fal.12:19  wakati nainua Kiapo hicho.
Leo MUNGU aliyemtuma Musa, Joshua, Eliya Mtishibi, Elisha, YESU, Petro, Paulo, Tito, Timotheo na Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi amelithibitisha jambo hili kuwa Kanisa la Siloam halitapasuka milele. Nilikuwa na hakika kuwa Kanisa la Siloamu haliwezi kupasuka, ndiyo maana nilikaa kimya hata wakati wa matusi mengi!

Hivyo,kila Kuhani aendelee na huduma Madhabahunii asiguswe halikadhalika kila Mkamilifu pia aendelee na huduma kanisani asiguswe. Aidha, waliokuwa wanamtukana MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote, ambaye ametengenezewa Jukwaa na Eliya Ad2
MUNGU wa Majeshi kama ilivyofunuliwa katika Mathayo 21:41 na 1Kor.15:28, wasirudie.
Nawatakia Ibada njema katika vituo vyenu vyote.
Tutawasiliana tena Wiki ijayo.

(Imesainiwa) 
Elisha Eliya Miaka1000
WAKILI WA MUNGU
1
The Pool of Siloam Church  - WAKILI WA MUNGU


No comments:

Post a Comment