MAJIRA NA NYAKATI

MAJIRA NA NYAKATI YA SIKU YA LEO.
Siku ya NNE.
Lango la 25.
Mwezi ABIBU.
Mwaka wa 6 wa UKAMILIFU NA UTIMILIFU WA ISAYA 2:2-4 NA ISAYA 60.
(29 October 2016)

THAMANI NA FAIDA YA MADHABAHU MOJA TU YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE


1.          Lugha na Nia Moja ya Kristo

Msomaji aliyeko Kanisani, atakumbuka kuwa lango la 3 Abibu, 4 niliita makuhani wote wa Gosheni na Nje na kusimamisha ibada ya lugha, nia na taifa moja ndani ya Kanisa kupitia 
MIAKA 1000 YA KUTAWALA NA KRISTO
Mwa 11:6.  Haikuwezekana jambo hili kufanikiwa kipindi kile kwa kuwa kulikuwepo bado na madhabahu nyingi mbovu ndani ya kanisa kama vile; madhabahu za ukoo, kabila, lugha, jamaa, cheo, tabia ya asili, sheria ya dhambi, na kadhalika.  

Lakini pia bado ndani ya makuhani na wakamilifu kulikuwepo na madhabahu za dini na madhehebu ikiwemo umimi.  Hivyo ilikuwa siyo rahisi kuvunja hizi madhabahu mbovu ili kujenga madhabahu ya kweli ndani yao ili kuleta lugha na nia moja ya Kristo, bila kufika kituo hiki cha madhabahu moja ya Aliyetuma wote vizazi vyote. Sasa hivi inawezekana kwa sababu ya Madhabahu hii moja tu ndani ya wafusi wa kweli.

2.          Madhabahu ya Kanisa bila kuzingwa

Kulikuwepo na madhabahu nyingi ambazo ni za kiwango cha uumbaji wote, lakini ni madhabahu mbovu, ambazo zilikuwa
zinasonga madhabahu ya Kanisa la kweli.  Madhabahu hizo ni pamoja na;

(a)        Madhabahu ya Kerubi (II Kor. 4:4)

Katika II Kor. 4:4 Neno linasema shetani ni mungu wa dunia hii. Hivyo ina maana ukiwa juu ya nchi na bahari ulikuwa unalazimika kusongwa na madhabahu ya kerubi, hata kama uko Kanisani. Madhabahu hii iko kila mahali na ndani ya kila kitu katika uumbaji wote kwa mujibu wa Mt 4:1-10 na Lk 4 5:5-9.

(b)       Madhabahu ya mwanadamu (Mwa 5:3)

Adamu wa kwanza alikuwa na madhabahu ambayo inamkamata kila aliyezaliwa na mwanamke.  Ndiyo maana hata  Yesu, anaitwa mwana wa adamu!  Madhabahu ilikuwa inalazimisha kila mmoja aliyeko juu ya nchi aitwe mwanadamu na MUNGU akawa ameachilia kila kitu chini ya miguu yake (Zab. 8:4-6). Bila Madhabahu ya Alliyetuma wote, madhabahu hii mbovu ya Adamu adisingevunjika!

(c)       Madhabahu ya Ibrahimu, Isaka na Yakobo (1Fal. 18 :36-38)

Katika 1 Fal 18:36-38, tunamuona Eliya Mtishbi (ambaye katika I Fal.17:1 na II Fal.2:9 anaongea kama MUNGU) akimwita MUNGU wake kupitia Madhabahu ya Ibrahim, Isaka na Yakobo.  Jambo hili tunaona likiendelea hadi kizazi cha tatu kupitia mwanamke msamaria aliyemuuliza YESU kama yeye ni mkubwa kuliko baba yao Yakobo (Yoh. 4:4-) lakini pia katika Mwa 12: 1-3; Mwa 26:3-5 na Mwa 35:9-15, MUNGU aliingia Agano kati yake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo la umilele.  Hivyo bila Madhabahu ya Aliyetuma wote vizazi vyote, ilikuwa haiwezekani kusimamisha Madhabahu ya Kanisa la kweli.

(d)       Madhabahu ya Torati ya Musa (Yoh. 9:28-29; Yoh 5:45)

Katika Mt 5:17 Yesu ambaye ni mwana wa MUNGU alithubutu kusema yeye hakuja kuvunja torati ya Musa. Hii ni kwa sababu torati hii hadi leo bado ndiyo inayoongoza kwenye taasisi zote za dunia na ulimwengu kupitia Kut. 7:1. Hivyo bila Madhabahu ya Aliyetuma wote, ilikuwa haiwezani hata kidogo kusimamisha Kanisa la kweli.

(e) Madhabahu ya Eliya Mtishbi (I Fal 18:33)

 Katika I Fal 18:33 tunasoma kuwa Eliya Mtishbi alijenga Madhabahu kwa kujaza maji (Neno la MUNGU) ndani ya mapipa manne, akiashiria kumiliki na kutawala vizazi vyote vinne!
Yesu pia anamkiri Eliya katika Mt 17:10-13 na Mk 9:10-12.  Hata Wayahudi wanamkiri Eliya katika Mt 27:45 -47 kwa hofu kubwa.  Nabii Malaki katika Mal. 4:4-6 anamkiri Eliya Mtishbi kwa hofu kuu ya MUNGU.   Ilikuwa kwa mantiki hiyo huwezi kuinua Kanisa la mwisho bila madhabahu ya Aliyetuma wote vizazi vyote kwa sababu ya nguvu ya madhabahu ya Eliya Mtishbi kizazi cha pili.

(f)        Madhabahu ya Yesu (Efe 1: 22:23)

Katika Efe. 1:22-23 tunasoma kuwa MUNGU Baba aliweka kila kitu chini ya YESU, ambaye kizazi cha tatu alifanyika kichwa cha Kanisa.  Hata hivyo katika kizazi cha nne, MUNGU alikusudia kupitia I Kor. 15:28 akija yeye mwenyewe awe kichwa cha Kanisa huku na mwana mwenyewe (Yesu) akiwa ametiishwa chini ya miguu ya MUNGU Baba.

Hivyo bila madhabahu hii ya Aliyetuma wote, ilikuwa haiwezekani kugusa madhabahu ya Yesu ambayo imeng’ang’aniwa na madhehebu yote ya kikristo bila kujua kuwa MUNGU anahamna kituo kulingana na majira na nyakati zilizonenwa kwenye kitabu chake ingawa habadiliki (Mal.3:6).

(g)       Madhabahu ya dunia na Ulimwengu (Dan 2:29-33)


Katika Dan 2:29-33 Neno linaonyesha kuwa dunia na ulimwengu walikuwa na madhabahu ya kudhibiti vizazi vyote vinne (kuanzia kizazi cha kwanza cha Musa hadi kizazi cha nne cha Eliya Ad2). Kwa mantiki hiyo, bila Madhabahu ya Aliyetuma wote vizazi vyote, ilikuwa vigumu mno kusimamisha Kanisa.
ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI.

SASA TUNAYO MADHABAHU MOJA PEKEYAKE YA MUNGU ALIYETUMA WOTE.


imekwisha kuwa!

No comments:

Post a Comment