FAILI LA HAKI YA GOSHENI KUFUNUA KANISA LA KWELI KWA MARA YA KWANZA NDANI YA UUMBAJI WOTE
WAKILI WA MUNGU
KIZAZI CHA MUNGU
MIAKA1000 ELIYA
LANGO LA 5 BULI 5 (22/5/2016)
SHUKRANI
Leo ni siku ya ajabu; vizazi vyote vilisubiri kushuhudia
siku ya leo kwa sababu ifuatayo kwamba: “Kila
mwenye haki ambaye yuko mahali hapa, leo anaondoka na faili la hatima yake
njema.” Nataka tumshukuru MUNGU kwa sababu kila mmoja ambaye yupo mahali
hapa, ana faili lake la hatma njema.
Agano la kila mmoja mahali hapa lina hatma njema, lakini
faili lako lilikuwa limefichwa mahali. Yaani karibu kila mmoja alikuwa
amebadilishiwa faili, sasa leo faili lako linarejea kwa Damu ya Haki, Kweli na
Hukumu!
Kuna maisha ambayo Kanisa tunaishi ambayo siyo ya kwetu,
leo unarejeshewa maisha hasa unayostahili kwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu.
Kuna maisha ambayo mlikuwa mnaishi wewe na kichwa wako au kanisa wako ambayo
siyo yenu, leo mnarejeshewa yale maisha ambayo ni “original”, yaani stahiki
yenu.
Kwa hiyo nataka tumshukuru MUNGU kwa kuwa lile faili la
Kanisa lisilokuwa na mawaa wala kunyanzi, kwa wewe mwenye haki, unahama nalo
leo unapokwenda Mlima wa Moto! Nadhani mnatambua kwamba huu ni mwezi wa Buli,
na katika Zek.1:1-5 Neno la MUNGU
linasema kwamba huu ni mwezi wa kila mmoja kumrudia BWANA.
Sasa siyo wewe tu bali kila kitu, mahali popote kilipowekwa
ambapo si penyewe (yaani si mahali pake), sasa kinarejea mahali pake. Kwa hiyo,
yule ambaye alikuwa amekaa na faili lako la hatma njema badala yako wewe,
ajiandae kupokea faili lake la uovu anaostahili. Yale mambo mazuri ambayo MUNGU
alikukusudia hata kabla hujaingia tumboni mwa mama yako, leo unaondoka nayo
hapa.
Usiseme kwamba nimezoea kusema maneno matamu matamu hapa,
lakini kile kipindi cha miezi minne cha mtihani kimekwisha! Niseme kwamba
ilikuwa ni lazima tupite mahali tulipopita; na kipindi cha kupita hapo mahali
tulipopita kimekamilika sasa. Sasa ni wakati wa kupata “certificate” (cheti) ya
ushindi “original”, yaani halisi.
Nikiwaona namna hii huwa najisikia kumshukuru MUNGU sana
kwa sababu kila ninayemuona hapa ameshinda; kwa sababu ilikuwa siyo rahisi
kwamba uje kunisikiliza hapa bila “mic” (kipaza sauti). Lakini nataka utambue
kuwa hata mimi sasa hivi nimepewa “mic” za mbinguni, hapa kwenye koo kuna
“amplifier” ya mbinguni, na malaika wapo hapa wanarekebisha mitambo kila
wakati. Nataka kila mmoja apaze sauti kumshukuru MUNGU kwa sababu siku ya leo
unaondoka na lile faili (la hatma njema), na utaona ukifika Mlima wa Moto,
utaanza kusikia faili la afya ya kiungu ndani yako.
+ Vile viungo ambavyo vilikuwa haviko sawa utaanza
kuvisikia vikijipanga sawasawa;
+ Hali uliyokuwa unaisikia kazini ambayo siyo sawa utaionaa
ikikaa sawa.
Nataka kila mmoja amshukuru MUNGU kwa kufika siku ya leo,
Mwezi Buli, siku ya tano ya mambo makubwa, ibada ya kwanza katika mwezi wa
kumrudia MUNGU.
Tunaposoma katika
Kum.28:13 Neno la MUNGU kwa wenye haki linasema kwamba “... utakuwa juu tu, wala hutakuwa chini, utakuwa kichwa tu wala
hutakuwa mkia.” Lakini ukiangalia hali halisi wengi walikuwa chini, sasa
ninamshukuru MUNGU kwa ibada ya leo kwamba, aliyekuwa chini kwa maonezi tayari
amekwenda juu! Na yule aliyekuwa juu, kwa kuwa alipandia mabega ya mwingine, na
kwa kuwa amepandia faili la mwingine, matawi yote yametereza na
yamekatikakatika! Hata shina la mti huo limeng’oka!
Nataka umshukuru MUNGU kwamba ulikuwa chini lakini tayari
umekweda juu! Maana, ni haki yako, na MUNGU alisema kuanzia Kizazi cha Kwanza
kwamba, kila mwenye haki lazima awe juu, na ni lazima awe kichwa; hata kama
wewe ni kanisa umevaa “skirt” (sketi), lakini wewe utakuwa kichwa kila mahali.
Nataka kila mmoja apaze sauti amshukuru MUNGU kwa sababu ukitoka hapa, naomba
usijisikie kuwa unatembea kwa mguu, hata kama kiatu chako kinaonekana kina
vumbi, hata kama mahali ulipopita leo kuna matope, bila kujali yote hayo, WEWE
UKO JUU! Hilo ni Neno la BWANA la leo! Haijalishi unatoka kwenye familia
maskini ya aina gani, hata kama babu na bibi na baba na mama walikuwa maskini
wa kutupwa, hiyo siyo “issue” (chochote, yaani haina maana) tena leo! Nataka
utambue sasa majira imefika kila aliyekuwa chini sasa anakwenda juu mradi
unatenda kwa haki!
Ukisoma Mwa.15:8, kuna
siku Abramu (yaani Ibrahimu wakati huo hajabadilishwa jina) alimuuliza MUNGU,
kwamba MUNGU tazama ninakwenda bila mtoto, na umenipa mali nyingi, nani atarithi
mali hii? MUNGU akasema utapata mtoto. Abramu akamuuliza tena, nitajuaje kwamba
nitapata huyo mtoto? MUNGU akasema, nipe hiki, nipe hiki, yaani MUNGU mwenyewe
akamwambia vitu alivyotaka vya kumpa kama sadaka. Sisi pia siku ya tano MUNGU
alituambia kwamba iko sadaka moja tu iliyosimama mbele yake.
Kwa hiyo wewe unayelifuata Agizo la Kweli, Maono ya Kweli,
na Ufunuo wa Kweli (na umeambiwa Ufunuo wa Kweli ni “original” na unatoka
kwenye kilindi cha moyo wa MUNGU kila asubuhi): kuja kwako hapa leo ni sadaka
imesimama mbele za BWANA kama ukumbusho; na kuamini kwako siku ya leo ni sadaka
imesimama mbele za BWANA kama ukumbusho. Hilo ndilo limesababisha sasa sadaka
zingine zote zilizokuwa zinasababisha wezi wa mafaili wakae badala yako
waondoke na wewe ukae kwenye nafasi yako. Hivyo nataka kila mmoja apaze sauti
amshukuru MUNGU kwa ajili ya hiyo sadaka moja peke yake ambayo imesimama mbele
zake kama ukumbusho milele inayosababisha leo uondoke na faili la hatma yako
njema!
Katika Isa.49:20
utakutana na watoto wengi wakikujia, vitu vingi vikikujia, na wewe utajikuliza
maswali:
+ Hivi hawa watoto wote walikuwa wapi;
+ Hivi haya magari yalikuwa wapi;
+ Hivi hii mitaji ilikuwa wapi;
+ Hivi haya maduka yalikuwa wapi;
+ Hivi hizi super maket zilikuwa wapi;
+ Hivi haya maisha mazuri yalikuwa wapi;
+ Hivi huku kupendwa na kila mmoja ananichangamkia kulikuwa
wapi? N.k.
Kumbe ni kwa sababu hatma yako imerejea! Usishangae
utakapoona kila mmoja anakupungia mkono wa heri. Hata yule aliyekuwa
anakuchukia atakuchekea, usishangae; Hata yule aliyekuwa hakusalimii ofisini
sasa atakusalimia; Hata jirani ambaye ulikuwa unaamini kwamba hakupendi, sasa
atakupenda.
Kwa maana ile hatma
yako ya kwanza, ile ya kupendeza, ya kuwakawaka imerejea! Kwa hiyo, ulikuwa
unaishi kama aliyefiwa, lakini sasa watoto wanakuja!
Unajua kwa nini hatma hii njema imerejea? Sababu ni hii,
kwamba tumefundishwa siku ya tano iliyopita kwamba yule MUNGU aliyetuma wote
vizazi vyote yuko hapa atekeleze maagizo yake yote.
+ Huu sasa ni wakati wa kutekeleza Agizo alilompa kerubi
kabla hajaanguka, la kusimama kwenye Neno, kwenye imani, kwenye utakatifu na
utii;
+ Ni wakati wa kutekeleza lile Agizo alilompa Adamu 1 kabla
hajaanguka, la kuilima na kuitunza Bustani ya Edeni, na kutoshirikiana na mti
wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa sababu hiyo vitu vizuri ni lazima vije.
+ Ni wakati wa kutekeleza lile agizo ambalo MUNGU alimpa
Musa la kuhakikisha kuwa kila mmoja anatoka kwenye:
• utumwa wa
magonjwa,
• utumwa wa
mizimu,
• utumwa wa
ujinga;
• utumwa wa
upumbavu; na
• utumwa wa
kila aina.
+ Ni wakati wa kutekeleza lile Agizo alilompa Eliya Mtishbi
kwamba kila mmoja atembee na madhabahu ya Kanisa;
+ Ni wakati wa kutekeleza lile Agizo ambalo MUNGU alimpa
YESU la kuhakikisha kwamba kila mmoja haonewi na ibilisi;
+ Ni wakati wa lile Agizo alilopewa Eliya AD2 la kumwabudu
MUNGU katika Roho na Kweli kutekelezeka, misingi mibaya kuvunjika ndani yetu,
na kila mmoja kusimama na Neno, Imani, Utakatifu na Utii; na pia kila mmoja
kujengwa juu ya msingi wa toba.
Sasa kwa kuwa huyo aliyetuma wote vizazi vyote, amesimama
hapa ingawa humuoni kwa macho, lazima wale watoto wote uliokuwa umeandikiwa na
MUNGU, warejee kwako! Kama umenielewa na unafahamu basi paza sauti ya kushukuru
nisikie!
Wiki iliyopita tulijifunza kwamba tumehamia rasmi katika Mt.21:41-43. Kuna maneno mawili makubwa
pale ninayoyaunganisha na msingi wa shukrani asubuhi ya leo.
+ Ni wakati wa kila mmoja amzalie MUNGU matunda kwa wakati; hapa kuna neno “matunda” na “wakati”. Hivyo kuna faili la matunda ambalo nataka kila
mmoja alipokee asubuhi ya leo, tena matunda yanayokuja kwa wakati. Wengine
mlikuwa mnapokea haki, lakini wakati mwingine inacheleweshwa, haiji kwa wakati.
Sasa MUNGU anataka, iwe ni mimi Miaka1000 au ni wewe, umzalie matunda kwa
wakati. Lakini, huwezi kuzaa matunda wakati hupokei matunda. Kuna wengine hata
mishahara hampati kwa wakati. Leo naanza na nyie ambao hampokei mishahara au
matunda kwa wakati:
• Kama ni
tunda la uponyaji unapokea sasa hivi;
• Kama ni tunda
la kuoa / kuolewa unalipokea sasa hivi;
• Kama ni
tunda la kupokea watoto unapokea sasa hivi;
• Kama ni
matunda ya “promotion” unapokea sasa hivi;
• Kama ni
matunda ya mtaji unapokea sasa hivi;
• Kama ni
matunda ya kazi utapokea sasa hivi;
• Kama ni kukonda
unajiona ni Michelin (kuna wengine wanachukia unene), wengine ni wanene, ikiwa
unataka wembamba unapokea sasa hivi. N.k.
Kundi la kwanza
Wale ambao wanapata taabu kupokea faili la matunda kwa
wakati. Ili ujue kwamba siyo Miaka1000 anaongea lazima upokee leo.
Kundi la Pili
Wale ambao kila wakati wanaona hatari ya kufa. Wakati
mwingine unaogopa kwenda kupumzika unaona kama utafia usingizini. Faili la
uzima wa milele ndiyo limerejea hapa. Kanisa leo limegeuka kuwa Treni
inayokwenda kwa kasi. Anayesimama kwenye reli hiyo anaondolewa mara moja. Ikiwa
tunaleta faili la matunda ni lazima tufute faili la mauti ambalo huwa
linaharibu matunda.
KUFUTA ROHO YA MAUTI NDANI YA TAIFA
Tumefuta roho ya mauti ndani ya Kanisa, lakini katika wiki
mbili mfululizo tumeona kwa kile kilichotokea kule Geita na Mwanza kwamba roho
hii ipo ndani ya taifa pia. Ni kazi yetu sisi Kanisa kufuta roho ya namna ile.
Tunafundishwa hivyo katika 1Tim.2:14, kwamba
kabla ya yote tuombee walioko madarakani na amani. Katika Yer.29:7 Neno linasema lazima tuombee amani mahali tulipo. Hivyo
sasa ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba mauaji ya namna ile hayatokei tena.
Nimekuwa pia nikiangalia kwa wale wanaoishi kwenye mapango ya Amboni, wanaishi
kwa wasiwasi sana. Ni wajibu wetu sisi Kanisa kuhakikisha kwamba tunafuta
wasiwasi, mashaka na hofu. Taifa ambalo lina madhabahu ya kweli halitakiwi
liishi kwa wasiwasi.
Unapoangalia matokeo ya toba, ukaona jambo la hatari, wewe
huangalii taarifa ya habari ufurahie na kuanza kujadili! Unaangalia taarifa ya
habari ili MUNGU aseme na wewe kuna tatizo gani ili ulifute.
Sasa matukio kama hayo, kama kule Sengerema, majambazi
waliingia nyumba moja wakawakatakata wote kwa mapanga, haitakiwi kurudia tena.
Jambo lingine lilitokea Mwanza mjini juzi, hata kama lilitokea msikitini,
lakini ni wajibu wetu kufuta mambo ya namna ile, kwa sababu tunataka wale
waokoke. Neno la MUNGU linasema MUNGU hafurahishwi na kifo cha mwenye dhambi (Eze.33:11). Hivyo ni wajibu wetu
kuhakikisha kwamba mambo hayo hayatokei tena.
Tutapita kwenye toba ili tulete polisi wa mbinguni waungane
na polisi wanaoonekana kwenye macho haya, wawakamate hawa waovu, na wengine
waliokuwa wanaota ndoto kufanya hivyo wasirudie tena!
Naomba nisahihishe kitu kimoja hapo. Wako wanaosema kwamba
Wakili wa MUNGU anasimama madhabahuni na kusema kwamba “kwa damu ya Miaka1000”
hii siyo kweli. Zab.89:14 imeweka
wazi kwamba msingi wa kiti cha MUNGU ni Haki na Hukumu, na kweli iko mbele
zake. Haki ni MUNGU, Kweli ni Neno / Kristo, na Hakumu ni Kanisa. Kwa hiyo
nikisema kwa damu ya MUNGU mwenyewe inatakasa pote toka Mlimani mpaka juu sana.
UJUMBE: FAILI
LA HAKI YA GOSHENI KUFUNUA KANISA LA KWELI KWA MARA YA KWANZA NDANI YA UUMBAJI
WOTE
Zek.1:1-5 “Katika mwezi wa nane ... BWANA wa Majeshi
asema hivi, nirudieni mimi asema BWANA wa Majeshi, ... msiwe kama baba zenu, ….
rudini na kuziacha njia zenu mbovu”.
Kwa hiyo asubuhi ya leo ninayo furaha ya ajabu kwa kuwa
faili la kila mmoja la kumrejea BWANA unalo mkononi tayari, na kila kitu kizuri
ambacho MUNGU alikikusudia kimerejea kwako kwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu.
Nataka nimshukuru MUNGU kwamba kila mmoja wetu hapa
anayetenda kwa haki, kama nilivyosema wakati wa kujenga msingi wa ibada ya
Neno, ninakuhakikishia kwamba utakaporejea nyumbani utajiona si wa kawaida.
Mahusiano yako na watoto, na mahusiano yako na majirani, kuanzia sasa hivi
yamebadilika. Mahusiano yako na bosi wako pia yamebadilika. Kwa hiyo faili pia
la taifa hili kulifunua Kanisa la kweli, limerejea.
Wale ambao mnafuatilia mafundisho, ukiangalia katika kile
Kitabu cha Haki na Kazi ya Nabii, utaona mahali ambapo ametamka kuwa Tanzania
ni Gosheni. Hivyo nikisema Gosheni nina maana ya Tanzania, nina maana ya taifa
ambalo lina nuru wakati ambapo kwingine kuna giza. Kila mahali ambapo Kanisa
hili litakwenda hakuna giza, bali kuna Nuru. Hivyo basi ile haki ya taifa hili
kufunua Kanisa la kweli, faili hilo limerejea.
Huko nyuma ulikuwa:
+ Ukiwa KKT ulikuwa unajua dini hiyo ilizaliwa Ujerumani;
+ Ukiwa Assemblies of God ulijua dhehebu hilo limezaliwa
Marekani;
+ Ukiwa Pentekoste ulijua kuwa dini hiyo ilizaliwa Sweden /
Scandinavia;
+ Ukiwa Aglican ulijua dini hii ilizaliwa Uingereza;
+ Ukiwa Baptist ulijua dini hiyo ilizaliwa Amerika (Marekani);
+ Ukiwa Presbyterian au Greek Orthodox, ulijua dini yangu
hii ilizaliwa Uyunani;
+ Ukiwa RC ulijua dini yangu hii ilizaliwa Urumi. N.k.
Leo kibao kimegeuka; tena kuna kipindi tulikuwa
tunaringishiana kwenye madhehebu, kwamba wewe dini yako ilitoka wapi? Wana
utajiri kiasi gani? Wanawaletea misaada kiasi gani? Tulikuwa tunaringishana kwa
sababu ya misaada. Lakini kuanzia leo tutazungumza kuhusu Kanisa la Kweli. Na
haki ya taifa hili kufunua Kanisa la kweli, faili hilo limerejea. Somo hili lilikuwa
halijafundishwa kwa sababu kila mmoja alikuwa amebadilishiwa faili.
Ukiona mataifa hayo leo ni matajiri ni kwa sababu yalizaa
dini na madhehebu. Wakati unazaliwa kwenye ile dini, ukaandikishwa,
ulipobatizwa ukaandikishwa, nafsi yako wewe hujui ilikwenda wapi! Ulipopokea
lile koti, ukafurahia ile suti ya msaada kwa mmisionari, nguvu yako wewe hujui
ilikwenda wapi! Leo nataka nimshukuru MUNGU kwamba Siloamu itakapokwenda
haipeleki ukoloni, bali inapeleka amani.
Nataka ujue leo unapotoka hapa, kuna ambao mliandikiwa
utajiri lakini mnaonekana maskini. Lakini leo ukitoka hapa wewe ni tajiri. Kuna
ambao mliandikiwa watoto wengi lakini mnaonekana hamjazaa hata mtoto mmoja; leo
ukitoka hapa ujue una watoto. Kuna wengine hapa mna vyeo vikubwa lakini mlikuwa
mnaonekana wa chini sana. Lakini nakwambia ukitoka hapa leo nafasi yako
imerejea. Kwa sababu lile faili la taifa kuwa na haki ya kufunua Kanisa la
kweli limerejea. Hakuna kitu MUNGU alisubiri kama hiki.
Kuna Kuhani aliyekusudiwa awe na abiria wengi, lakini hata
wawili walikuwa hawafiki. Kila wakati alikuwa anaomba abadilishiwe kituo, leo
kibao kimegeuka.
Ni kwa sababu abiria wa huyo Kuhani walikuwa kwenye soka na
wengine walikuwa kwenye volleyball, wengine walikuwa bado kilabuni, wengine
walikuwa bado RC, na wengine walikuwa bado wako KKT, leo wanakuja! Kuna wengine
mlikuwa mmeandikiwa masupa maketi makubwa makubwa, lakini hata ukianzisha
kioski, kilikuwa hakidumu, kwa sababu ulikuwa umebadilishiwa faili. Leo
limekuja la kwako!
Ushuhuda
Thamani Kizazi cha Nne, muimbaji, siku moja aliniuliza
swali, kwamba mimi nimepewa kuwakamilisha waimbaji. Mbona mimi mwenyewe
sijakamilika? Sasa leo amepata wa
kumkamilisha!
Kwa hiyo wewe ambaye ulikuwa unaona uko chini, kumbe uko
juu. Wewe uliyekuwa unajiona mwembamba, kumbe ni mnene. Wewe uliyekuwa unajiona
mfupi kumbe ni mrefu. Wewe uliyekuwa unajiona maskini kumbe ni tajiri. Wewe
uliyeambiwa una uso mbaya kumbe una uso mzuri. Kwa maana faili limerejea.
KANISA HILI
LINAFUNULIWAJE?
Kanisa la kweli lisilo na mawaa wala kunyanzi
linafunuliwaje?
Katika Mt.16:18
neno linasema “... nami nakuambia wewe
Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu na malango ya kuzimu
hayatalishinda”! Lakini Kanisa hili Warumi walilikamata kwa sababu kaburi
la Petro liko kwa Warumi. Baada ya YESU kutamka hilo Neno basi ikawa
walipofanikiwa kumuweka Petro msalabani, miguu juu kichwa chini, Kanisa hilo
mpaka leo halijaonekana.
Lakini pia walipofanikiwa kumpeleka msalabani YESU, na
Askari wa Kirumi akamchoma mkuki, pakatoka maji na damu katika Yn.19:34, basi kauli hii na Kanisa hili
lililotambulishwa kwa mara ya kwanza, halikuonekana tena! Tulichokuwa tunakiona
ni dini na madhehebu.
Katika
Mdo.11:26 Neno la MUNGU linasema “hata alipokwisha kumuona … wakakusanyika
pamoja na wanafunzi waliitwa Wakristo kwa
mara ya kwanza ...”. Hapa Kanisa
lilitambulishwa kwa mara ya pili, na anayeongelewa hapo ni Mtume Paulo ambaye
alipokea wokovu katika Mdo.9, na
katika Mdo.13 tunaona akiitwa kwenda
kila mahali. Kanisa hili pia lililotambulishwa kwa mara ya pili na Mtume Paulo,
lilitekwa nyara na dunia. Hatukuliona tena, ila tunasoma juu ya makanisa saba
ya Asia ambayo ukisoma katika Ufu.2&3
tunaona yote siyo makanisa bali ni dini. Isipokuwa lile la Filadelfia, ambalo
nalo Neno linasema lilikuwa na Neno kidogo, hivyo likafifia.
Kwa
mara ya tatu katika kitabu cha Mt.21:40
“ ... basi atakapokuja yule BWANA wa
shamba la mizabibu atawatendaje wale wakulima? Maana tukisoma katika kitabu
cha Mt.21:34-35 tunaona habari za
MUSA, Mt.21:36 tunaona habari za
Eliya Mtishbi, Mt 21:37-39 tunaona
habari za YESU Kizazi cha Tatu.
Katika Mt.21:40
ni habari za Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi, maana ndiye aliyekuja Kizazi cha Nne
akiwa amemleta MUNGU, akalitambulisha Kanisa kwa mara ya tatu. Ile siku ambapo
tulianza miaka 1000 ya kutawala na Kristo akasema Siku 1, Wiki 1, Mwezi 1, na
Mwaka 1. Lakini pia sura halisi ya Kanisa lisilo na mawaa wala kunyanzi,
halikuonekana kwa kuwa tulikuwa bado tunashitakiana, tulikuwa bado
tunanyosheana vidole, tulikuwa bado tunatukanana bila aibu na kupigana
ngwala.
Kanisa ambalo MUNGU analifunua sasa halina mawaa wala
kunyanzi, mahali pasipo na mauti wala kifo. Mahali ambapo faili la kila mwenye
haki la hatma njema limerejea.
Kwa hiyo, nataka ujue kwa nini ujumbe huu umekuja leo.
Katika Mt.21:34-39 tunazungumza juu
ya Israeli ya mwilini, ambako ndipo MUSA, Eliya Kizazi cha Pili na YESU
walipokuwa, waliopokea maagizo matatu kwa vizazi vitatu vya kwanza. Ile injili
iliyotoka mashariki ya kati (Israeli ya mwilini), ikaenda Ulaya, ikaenda
Amerika, ikaja Afrika na Asia, ilikuwa ni feki. Ufunuo utakaotoka hapa kwenda
sehemu nyingine ndiyo wa kweli.
Mara nyingi unapozungumzia dini na madhehebu ya Kikristo,
si mara nyingi utasikia Israeli ya mwilini inazungumzwa. Nimesema hivi,
unapozungumzia RC unasema juu ya Urumi wala huzungumzii Israeli ya mwilini;
ukizungumzia Anglican unasema juu ya Uingereza wala huzungumzii Israeli ya
mwilini; ukizungumzia Assemblies of God unasema juu ya Amerika wala siyo
Israeli ya mwilini. Ukizungumzia KKT unasema juu ya Ujerumani, wala siyo
Israeli ya mwilini. Ukizungumzia Pentekoste, unasema juu ya Sweden /
Scandinavia wala siyo Israeli ya mwilini. Ukizungumza Greek Orthodox au
Presbyterian, unasema juu ya Uyunani wala siyo Israeli ya mwilini.
Israeli ya mwilini walishasahaulika kwa sababu ya Injili
iliyokuwa feki yenye misingi mibaya. Ninachosema leo, limekuja faili la haki ya
taifa hili kufunua Kanisa la Kweli lenye Agizo la Kweli! Kwa hiyo kuna kazi
tunayotakiwa kufanya ili na sisi tusisahaulike, tusije na sisi tukafunua dini
au dhehebu badala ya Kanisa.
Tutambue
jambo moja, kwamba kuna Makuhani ambao tumewatuma kule nje ya nchi, wao
wamesajili Kanisa siyo dini. Lakini wanahangaika sana kwa sababu Neno katika Mt.21:41 lilikuwa bado
halijatimia.
Ndiyo maana walioko nje walikuwa wanafanya kazi kwa ugumu
kwa sababu sisi tulikuwa bado hatujasajili Kanisa.
Hapa
hatuwezi kukwepa kugaragara kwa siku saba. Kila mmoja leo akitoka hapa, kwa
kuwa amepata zawadi, maana MUNGU hawezi kukupa zawadi bure, anataka akupe kazi.
Ili hawa tuliowatuma kwenye mataifa, wasitaabike, leo tumwambie MUNGU tunatoka
vitandani kwa siku 7. Ila wale ambao mumeolewa na akina baba ambao hawajaokoka
msitoke kitandani, maana watawashangaa. Lakini wewe ambaye kichwa wako
ameokoka, na wewe kichwa ambaye kanisa wako ameokoka, utoke kitandani kwa siku
saba kuanzia leo. Ili Faili la Haki ya
Taifa hili kufunua Kanisa la kweli lionekane waziwazi ndani ya siku 7. Nataka
niwaapie leo, ukiona faili hili umelipokea, utashangaa jinsi ambavyo uchumi
utavyobadilika kuwa mzuri kuanzia wa kaya, kijiji, kata, tarafa na wa kila
aina. Kila kitu ambacho tumewahi kutafuta lazima tukione! Kila uzuri ambao
tumewahi kuutafuta lazima tuuone!
Mataifa mnayoona yameendelea, yalikuwa na haki ya kuzaa
dini na madehebu. Ukiona Uarabuni wanaringa ni kwa sababu walizaa dini. Ukiona
Ulaya wanaringa ni kwa sababu walizaa dini. Ukiona Amerika wanaringa ni kwa
sababu walizaa dini.
Sisi siyo dini, ni Kanisa ambalo tutashangaza Uumbaji wote!
Hizi “struggle” tunazoziona (yaani haya mahangaiko mnayoyaona, hamtayaona
tena) hatutaziona tena.
Kwa sababu MUNGU atakuja akae mzima mzima! Na mataifa
ambayo tumepeleka Kanisa, vita dhidi ya Kanisa itakwisha. Umasikini utakwisha,
na wale makuhani hawataishi tena maisha ya shida.
Sasa imekuwa tatizo, wakati mwingine wanaomba masaada huku;
wakati mwingine wanaomba chakula kutoka huku, wakati ambapo huu siyo msingi wa
Kanisa. Naona kama na sisi tunataka kuanzisha umisionari. Maana wanakwenda kule
halafu wanaomba msaada huku, ina maana wale wasibarikiwe. Sisi hatujapeleka
jambo hilo (yaani umisionari). Lakini kinachosababisha wahangaike, ni kwa
sababu sisi bado tulikuwa hatujafunua hilo faili la haki ya taifa hili kufunua
Kanisa la Kweli la Aliyetuma wote Vizazi vyote, linalotekeleza maagizo yote ya
MUNGU!
HITIMISHO
Unaelewa kwa nini leo MUNGU amekupa zawadi? Kwa wale
waliowahi sana, leo MUNGU ametupa zawadi ya faili la Hatima njema na tunaondoka
na faili la zawadi hiyo ambayo unatakiwa ukaifanyie kazi kwa siku 7 ukiwa
chini, yaani utoke kitandani upumzike chini.

No comments:
Post a Comment