THAMANI NA FAIDA YA
KUSIHI KWENYE KITUO CHA
LAIYETUMA WOTE
VIZAZI VYOTE
LANGO LA 12 ETHANIMU 5 ( 1 May 2016)
MIAKA1000 ELIYA
WAKILI WA MUNGU
KIZAZI CHA NNE
SHUKRANI ♯1
Ninamshukuru MUNGU kwa ajili ya toba ya
kugaragara ambayo nimeikuta inaendelea mahali hapa. Sote tunajua kilichotokea
katika Esta 4:3 kwa Wana wa Israeli
Kizazi kile cha Pili walipotubu kwa kugaragara, kwamba mauti ilifutika. Kwa
hiyo hata sisi leo, chochote kilichokuwa kimepangwa kinyume na Kanisa, kwa Toba
hii kimefutika kwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu!
Kwa hiyo nataka wote tumuinue MUNGU kwa
kumshukuru tukijua kwamba mahali popote ulipokuja na wasiwasi, mashaka, na
hofu, kwa toba hii tuliyoanza nayo mauti hiyo imefutika moja kwa moja! Kwa hiyo
mshukuru MUNGU kwamba mauti iliyokuwa imeagizwa katika ibada hii haipo; Hata
kama umekuja unaumwa au unajisikia vibaya ina maana kwa toba hii maumivu hayo
yamefutika!
SHUKRANI ♯2
MUNGU katika Lk.10:19 ametupa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka kwa maana ya
hila na maumivu.
Sasa kupitia toba hii nakuunganisha na:
+ Mamlaka ya kuishi;
+ Mamlaka ya uzima;
+ Mamlaka ya uhai;
+ Mamlaka ya ulinzi wa MUNGU;
+ Mamalaka ya Ibada ya leo;
+ Mamalaka ya uponyaji;
+ Hata kama umekuja na maumivu basi ile
mamlaka ya uponyaji tunaiyosoma katika
Lk.10:19 iingie kwako;
+ Hata kama jana ulipata hasara, basi sasa
mamlaka ya kupata faida iingie kwako sasa hivi;
+ Hata kama umekuja na huzuni, mamlaka ya
furaha iingie kwako kupitia hiyo toba; N.k.
SHUKRANI ♯3
Siku ya tano iliyopita, tulijikabidhi na
tulimkabidhi aliyetuma wote vizazi vyote kila kitu kama neno linavyosema katika Mt.21:4043. Hivyo Tumshukuru MUNGU kwa kuwa sasa Kanisa linaishi mahali pa Mt.21:40-43, ikimaanisha kwamba:
+ Magonjwa hayatakiwi yawepo tena;
+ Umaskini hautakiwi uwepo tena;
+ Ufukara na mizimu hautakiwi uwepo tena;
+ Giza, ukiwa na utupu havitakiwi
kuonekana hata kidogo tena; n.k.
Haya yote hayatakiwi kuwepo kwa sababu
tumejikabidhi kwake yeye Aliyeumba wote,
akawatuma kuanzia Kizazi cha Kwanza mpaka Kizazi cha Nne. Ina maana sasa hivi
kila kitu kimo mikononi mwake! Kwa hiyo yale yote yaliyokuwa yanakuliza,
yanakusikitisha, anayaona na anauwezo wa kuyafuta mara moja: + Hila yoyote
uliyowahi kufanyiwa haiwezi kuwepo tena, maana uliyejikabidhi kwake yuko juu ya
hila;
+ Dhuluma yoyote uliyowahi kupata haiwezi
kuwepo tena, maana huyo uliyejikabidhi kwake yupo juu ya dhuluma ya aina yoyote;
+ Kila aina ya mti wa ujuzi wa mema na
mabaya uliokuwa unakuzonga umekauka moja kwa moja, maana aliyetuma wote vizazi
vyote unatembea naye kila mahali. Kwa
maana umehamia mahali pake yeye, na Ibada hii inafanyikia mahali pake
yeye aliyetuma wote. Ina maana mifupa yako, damu yako, na kila kitu ulicho
nacho, pamoja na akili yako, hisia yako, hiari yako, matamanio ya moyo wako,
vyote vipo mahali pa aliyetuma wote!
Kwa hiyo kama kulikuwa na bacteria au
virusi huko ndani lazima waungue kwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu! Ole,
mnyama, kahaba mkuu, na behewa la nje haviwezi kuwepo tena.
Nataka kila mmoja amwambie MUNGU,
ninakushukuru kwa sababu: nimekutana na matatizo, huzuni, na shida za hapa na
pale, lakini haitatokea tena kwa sababu sasa kila kitu sasa kimekabidhiwa
kwako:
+ Mimi mwenyewe nimekabidhiwa kwako;
+ Familia yangu, biashara yangu, kazi
yangu, na agano langu vyote vimekabidhiwa kwako wewe uliyetuma wote vizazi
vyote. Kwa hiyo yale yaliyowatokea vizazi vilivyopita, wewe hayatakutokea tena.
Kwa mfano haya yafuatayo hayatatokea tena:
= Yn.18 (Kukamatwa
kwa YESU) imefutwa;
= Mdo.4 (Kukamatwa
kwa Petro) imefutwa;
= Mdo.16 (Kukamatwa
kwa Paulo) imefutwa;
=
Mt.4 (YESU kupelekwa na Roho Mtakatifu kwa shetani ili ajaribiwe) imefutwa;
= Mwa.4:1-10 (Kuuawa kwa Habili mwenye haki) imefutwa; = Mt.21:33-39 (Waliotumwa wote kuishia
njiani) imefutwa.
Kwa jambo hilo mwambie MUNGU nakushukuru
kwa sababu nimekuelewa.
SHUKRANI ♯3
Nilikuwa najiuliza
Isa.65:16, inayosema kuna kipindi kitakuja:
+ Anayeapa, aape kwa MUNGU wa kweli peke yake;
+ Anayefanya biashara ili abarikiwe,
abarikiwe kwa MUNGU wa kweli peke yake;
Sasa imefika, baada ya kila kitu kuwa
kimekabidhiwa kwa MUNGU Aliyetuma wote! Wewe mwenyewe ni mali yake, wabaya na
wema wote sasa wapo kwake. Ina maana sasa hivi yeyote asiyeapa kwa MUNGU wa
kweli, hawezi kufanikiwa! Baada ya ibada ya siku ile ya tano:
+ Yeyote anayekuendea kwa mganga
hawezi kufanikiwa; + Kila mafanikio
lazima yawe kwa MUNGU wa kweli.
+ Yeyote anayekutishia, kama siyo kwa
MUNGU wa kweli hawezi kufanikiwa.
Hivyo
Isa.65:16 imetimia ni wakati wa kutafuta jibu kwa MUNGU wa kweli peke yake,
ni wakati wa:
= MUNGU kukimbiliwa;
= MUNGU kufuatwa;
= MUNGU kuabudiwa;
= Kila mahali mwenye haki atakapokuwa
MUNGU lazima aonekane hapo.
Ni wakati wa kila anayefanikiwa, afanikiwe kwa MUNGU wa
kweli:
+
Hakuna uganga tena;
+ Hakuna ushirikina tena;
Kwa sababu
+
Hakuna magonjwa tena; amesimama MUNGU + Wasiwasi, mashaka na hofu wa kweli wala vita hakuna tena.
Mwambie MUNGU nakushukuru kwa kuwa:
+ Nilikuwa na shida nyumbani kwangu, kumbe
kwa kuwa mimi nina MUNGU wa kweli, na ibada hii inaongozwa na wewe MUNGU wa
kweli, najua hiyo shida nikirudi utakuwa umeishughulikia;
+ Nilikuwa na tatizo kazini kwangu, lakini
kwa kuwa yule aliyeniletea shida alikwenda kwa mganga, na anayekwenda kwa
mganga siyo MUNGU wa kweli, ina maana mimi nimeshamshinda tayari.
SHUKRANI ♯4
Isa.42:18 – Upofu wa
Rohoni
Katika kifungu hicho neno la MUNGU
lilikuwa linasema, wale ambao wamekuja kwa MUNGU wa kweli ndio hao wanaendelea
kuwa vipofu wasimuone. Lakini sasa hivi huo upofu wa rohoni umeondoka; hata ule
uziwi wa rohoni nao umeondoka. Kwa kuwa
kila neno linalotamkwa hapa madhabahuni lazima litimie, ni lazima utafunguka
macho tu!
Zek.3:3-7 – Mavazi
machafu
Hapa inaonyesha kwamba hata kama ni mwenye
haki kuna namna ambayo ulikuwa unaweza kuvikwa mavazi machafu yakakupata.
Nataka tumshukuru MUNGU kwamba kwa kuwa yupo yeye mwenyewe, mavazi machafu
uliyokuwa ukivikwa, hayawezi kukupata tena! Ile mishale uliyokuwa unatupiwa
haiwezi kupenya kwa yule uliyemtanguliza mbele yako.
Rum.6:16 - Utumwa wa
rohoni
Neno la MUNGU linasema hapa kwamba kuna
vitu unavipenda kuliko kawaida, na ulikuwa umegeuka kuwa mtumwa wa vitu hivyo.
Au kuna kitu unakipenda mpaka ukageuka kuwa mtumwa wa jambo hilo. Kuna mahali
unapenda kwenda, lakini hutaki kupaacha hata kama umeshahama kituo, mpaka
ukageuka kuwa mtumwa. Sasa mshukuru MUNGU aliyetuma wote vizazi vyote kwamba
amekutoa katika utumwa huo. Wewe mwenyewe unajijua ni kitu gani ulikuwa unakipenda
kuliko hata MUNGU; lakini MUNGU asa amekutoa mahali hapo.
Hos.4:6 – Kukosa
maarifa
Neno
la MUNGU linasema kuwa tulikuwa tunapotea kwa sababu ya kukosa maarifa. Lakini
sasa chanzo cha maarifa ambacho ni “kumcha MUNGU” kitaonekana. Ikimaanisha kwamba, hatutapotea tena
wala hatutaangamia tena, maana chanzo cha maarifa sasa tunatembea nacho!
Mdo.3:1- Uwete wa
Rohoni
Katika
Mdo.3:1- kulikuwa na uwete wa rohoni, yaani ile tabia ya kutochukua hatua,
sasa MUNGU ameuondoa. Mshukuru MUNGU kwamba mambo hayo yote ameyaondoa.
SHUKRANI ♯5
Mwa.8:4 – Kanisa
kuwa juu tu
Tumshukuru MUNGU kwa Kanisa kutoka chini
kwenda juu. Katika Mwa.8:4 neno la
MUNGU linasema katika mwezi wa Ethanimu ndipo safina ilipotua juu ya milima
mirefu. Huu ni mwezi wa Ethanimu, na safina maana yake ni Kanisa. Lazima sasa
Safina itue sawasawa.
Neno la MUNGU katika Kum.28:13, kwamba mimi na wewe ambao ndio Kanisa tutakuwa juu tu,
hatutakuwa chini; kwamba tutakuwa kichwa tu, hatutakuwa mkia! Tumshukuru MUNGU
kwamba katika mwezi huu wa Ethanimu mwaka wa Tano (5), jambo hilo
limetokea. Hata kama jambo hilo
lilitakiwa kutokea lango la 17, hata
kama lango la 17 litafika wiki ijayo, lakini nataka uamini kuwa MUNGU tayari ameshatenda. Mshukuru
MUNGU kwa nguvu zako zote kwamba haya yote lazima uyaone. Kumbuka wakati wa
Kizazi cha Tatu Kanisa lilipotajwa kwa mara ya kwanza na YESU (Mt.16:18), dunia waliiba! Kanisa
linavyokuwa juu ina maana ni:
+ Wewe uko juu;
+ Agano lako liko juu;
+ Familia yako iko juu;
+ Biashara yako iko juu;
+ Afya yako iko juu;
+ Na kila unachotenda kiko juu.
SHUKRANI ♯6
Neema ya Wakili wa
MUNGU
+ Tumshukuru MUNGU kwa Neema ya Wakili ya
MUNGU iliyotubeba kwa miezi sita (6) sasa ya mtikisiko wa Kanisa.
+ Jana MUNGU alinionyesha kitu cha ajabu,
alinionyesha ile Neema ya Wakili wa MUNGU. Rohoni nilikuwa nimewabeba mgongoni,
wengine tumboni na wengine mabegani kwa jinsi mlivyo wengi. Lakini nikamuuliza,
mbona MUNGU tulipoingia Siku 1, Wiki 1, Mwezi 1, na Mwaka 1, Eliya alifuta
neema hiyo, wote tukawa tunaishi kwa ufahamu, imerudije?
+ Akasema katika kipindi hiki cha miezi
sita ilikuwa ni lazima arudishe neema hiyo, maana wengine mlikuwa hamuwezi
kuvuka wenyewe. Baada ya Kanisa kufikiwa kwenye kituo cha 1Kor.2:610 ilibidi MUNGU arudishe Kanisa kuishi kwa Neema ya
Kiongozi wao ili kulivusha Kanisa kwa kipindi ambacho Kanisa limepata mtihani
mgumu kuliko kipindi chochote.
+ Lakini sasa mambo yamefunguka, na kwa
kuwa tumehamia Mt.21:41-43, mahali ambapo Aliyetuma wote anaishi, miezi sita (6)
imekwisha, na kwa kuwa pia Kanisa limefunuliwa na kuwekwa wazi ndani ya Uumbaji
wa Rohoni na Uliofunuliwa, basi nawarudisha kuishi kwa ufahamu wa Neno. Kabla
sijawarudisha, tumshukuru MUNGU kwanza kwa ajili ya neema hiyo. Leo
tumehamishia Neema hii ya wakili wa MUNGU
Mt.21:40-43 ili Wakamilifu na Makuhani wote waishi hapo kwa raha.
TOBA YA KWELI KWA AJILI YA MAMBO YALIYOKUWA YANALETA LAANA JUU YA KANISA
Kumbuka ibada ya Siloamu haikamiliki bila
toba. Namshukuru MUNGU kwamba leo tumeanza na toba na tunaendelea na toba;
maana toba haiishi, ni endelevu. Leo tunatubu kwa ajili ya mambo yaliyokuwa
yanaleta laana kwa Kanisa:
(1) Kumkataa
Mpakwa Mafuta;
(2) Kunyanyasa
wadogo ndani ya kundi;
(3) Kufanya
dhambi kuliko vizazi vilivyopita;
(4) Kutomjua
MUNGU (yaani kutoijua tabia ya MUNGU);
(5) Wenye
Haki kuona MUNGU hayupo na kuendelea kukiri hivyo;
(6) Kuchoma
moto Sanduku la Agano bila aibu; na
(7) Matusi
ya Wakamilifu na Makuhani.
UKOMBOZI WA MASOMO YOTE YA MSINGI NA JENGO NA
KUYAHAMISHIA MT.21:40-43
Kuhamishia kila kitu
anapoishi MUNGU Mt.21:40-43
Kwa
sababu sisi wote na MUNGU aliyetuma wote tunaishi Mt.21:40-43, nataka tuhamishe masomo yote tuliyojifunza tangu 2003
mpaka leo, tuyahamishie hapo tunapoishi. Hata kama yaliibiwa yataletwa sasa
hivi na malaika wa marejesho; Hata kama
yalichomwa moto yatahuishwa sasa hivi kwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu!
Leo tunakomboa:
= Agizo, Maono na Ufunuo;
= Kuvunja Misingi Mibaya yote;
= Madhabahu ya Kanisa;
= Majira na Nyakati za Kanisa;
= Mbingu Mpya na Nchi Mpya;
= Maachilio ya Kanisa;
= Kutotembea Njia Moja na Waovu tena;
= Siku 1, Wiki 1, Mwezi 1, na Mwaka 1;
= Neema;
= Toba ya Kweli;
= Maono ya MUNGU;
= Upendo wa MUNGU;
= Chanzo, Msingi, Limbuko na Kitovu cha MUNGU;
= Thawabu ya MUNGU;
= Wivu wa BWANA;
Masomo Baada ya
Unyakuo:
= Kanisa Kupatanishwa na Nafsi ya Tatu ya MUNGU;
= Utawala wa Kristo;
= Ufufuo wa Kwanza;
= Kuunganisha Msingi na Jengo;
= Umilele;
= Mbegu ya Rohoni;
= Toba ya Vizazi Vyote;
= Sauti Moja ya MUNGU wa Majeshi;
= Kusudi la MUNGU la tangu Mwanzo;
= Uumbaji Mpya;
= Mji Mtakatifu;
= Visima vya Mambo Mazuri Peke yake;
= Kuungana na Kiuno cha MUNGU wa Majeshi;
= Asili ya MUNGU;
= MUNGU, Kristo na Wakili wa MUNGU kulifunua Kanisa kwa
Neno bila Mawaa; na,
= Kumkabidhi MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi
Vyote kila kitu ndani ya Uumbaji.
UKOMBOZI WA MIKOA YOTE YA GOSHENI
+ Dar es salaam è Jiji
la siloam;
+ Pwani è Agano la Urithi wa Isaka
Kizazi cha MUNGU;
+ Tanga è Agano la Kweli;
+ Kilimanjaro è
Ararati;
+ Arusha è Elimu MUNGU wa Majeshi;
+ Manyara è Filadelfia;
+ Mara è Mito ya Toba;
+ Mwanza è Karmeli;
+ Simiyu è Hermoni;
+ Singida è Wivu wa BWANA;
+ Shinyanga è Haki, Amani na Furaha;
+ Geita è Kazi za Dhahabu;
+ Kagera è Matenegenezo;
+ Kigoma è Jiji la Eliya;
+ Tabora è Rhema;
+ Dodoma è Ufahamu wa Neno la Ufunuo;
+ Morogoro è Mlima wa Neema Kubwa;
+ Iringa è Ufunuo wa Kristo;
+ Mbeya è Gibeoni;
+ Sumbawanga è Havila;
+ Katavi è Njia ya Watakatifu;
+ Njombe è Mamlaka ya MUNGU wa Majeshi;
+ Ruvuma è Shilo-na-Zaidi;
+ Mtwara è Hebroni;
+ Lindi è Isa.2:2
+ Zanzibar è Kanaani;
+ Pemba è Siku ya Kristo; na
+ Tanzania è Gosheni
UJUMBE WA LEO: THAMANI NA FAIDA YA KUISHI KWENYE KITUO CHA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.
1. Maswali
yote kujibiwa
Maswali yote ambayo uliwahi kujiuliza
kuhusu MUNGU unayemfuata, sasa yanajibiwa.
Zab.121:1-2
+ Katika Zaburi hii neno linasema, “nitayainua macho yangu niitazame milima;
msaada wangu utatoka wapi?
Msaada
wangu utatoka kwa BWANA; aliyeziumba Mbingu na Nchi”. Kulikuwa na maswali
mengi sana, ndani ya mioyo ya wakamilifu na makuhani, maswali ya siku nyingi
ambayo yalikuwa hayajawahi kujibiwa. Nitakuonyesha baadhi ya mistari ambayo
wengi wakisoma walikuwa wanaona ni maswali maana walikuwa hawaoni kama
inatekelezeka.
+ Lakini kwa kuwa huyu MUNGU Aliyetuma
wote tuko naye, tumejikabidhi kwake, maagano yetu tumeyakabidhi kwake, familia
zetu tumezikabidhi kwake, na biashara zetu tumezikabidhi kwake, maswali yako
yote sasa lazima yajibiwe. Kipindi hiki siyo tena kutazama juu milimani, bali
uko naye huyo anayekujibu wewe!
Isa.62:1-3
- Lini hasa sisi Wenye Haki tutaonekana ni Taji la MUNGU?
+ Neno hapa linasema kwamba MUNGU kiti
chake hakikaliki mpaka ahakikishe haki yako imekuwa kama mwangaza. Msitari wa
tatu anasema wewe ni taji mkononi mwake. Lakini wengi walikuwa wanajiona kama
majivu? Wengi walikuwa wanajiona kama hawafai. Lakini nataka nikuhakikishie
kuwa kuanzia sasa hivi, huyo MUNGU unayefuatana naye, aliyetuma wote vizazi
vyote, hatakubali uonewe tena maisha yako yote! Kwa hiyo, kama ulikuwa na
maswali kuwa huyu MUNGU ninayemuabudu yuko wapi; ninayeamka alfajiri kwenda
kumuabudu, kwamba mbona simuoni? Usiulize swali hilo tena. Utayaona majibu yake
sasa hivi kwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu!!
Isa.41:11-13
- Hivi ni kweli wale maadui watatu (maradhi, ujinga na Umaskini) utafika wakati
tusiwaone tena?
+ Hapa utakuta inaonyesha kwamba kila aina
ya adui hutamuona tena.
+ Kumekuwa na maadui watatu ambao wamekuwa
wakitamkwa katika taifa hili kwa muda mrefu, k.m. maradhi, ujinga na
umaskini.
+ Leo umesikia taifa lote na mikoa yote tumeihamishia
mahali MUNGU alipo, utaona haya yakifutika sasa hivi kwa Damu ya Haki, Kweli na
Hukumu.
Maana yule aliyetuma wote vizazi vyote
hatumi tena, usimwangalie aliyetumwa, sasa hivi hayupo bali yupo yeye mwenyewe!
Wala usimtazame (usimtafute) milimani, bali upo naye hapo “ndani ya moyo wako”!
Kuna chumba chake ndani ya moyo wako! Yule aliyesema, “Mimi naishi mahali pa
juu palipoinuka, na ndani ya moyo uliotubu na kunyenyekea”, sasa yupo nyumbani
kwako!
+ Kituo tulichopo ni kituo cha ajabu
kabisa. Kizazi cha Kwanza hawakufika hapo! Kizazi cha Pili hawakufika hapo!
Kizazi cha tatu hawakufika hapo! Sisi tumepata neema ya kufika hapo! Kuanzia
leo uamini kuwa ndivyo ilivyo.
+ Umepatwa na ugonjwa siku nyingi, na neno
linasema kwamba utakunywa sumu na vitu vya kufisha hutakufa, lakini wewe unaona
kama unakaribia kufa! Leo nina habari njema kwako! Kama hukufa wiki iliyopita,
hutakufa tena! Maana sasa hivi umeshakabidhiwa kwa chanzo cha uhai! Usifikiri
ni maigizo, wengi wanasema hawa wa madhabahuni
wamezoea kusema maneno matamu matamu, Sivyo, hii ni halisia!
Kut.19:4-5
– Lini hasa Wenye Haki tutakuwa Tunu kuliko Makabila yote duniani?
+ Katika Kut.19:5, neno la MUNGU linasema kwamba tumeahidiwa muda mrefu
sisi kuwa TUNU kuliko makabila yote.
Lakini wengi wamekuwa wakijiona sivyo:
+ Akiangalia ngozi yake anaona kama amekwisha kabisa;
+ Akiangalia biashara yake anaona karibu anakufa na
njaa;
+ Akiangalia kazi yake anaona kama karibu anafukuzwa;
Leo nataka nikuhakikishie kuwa kwa kituo
hiki wewe sasa ni TUNU! Mimi nataka
niwaapie, mtaanza kuona mataifa mliyokuwa mnayaogopa yanakuja hapa kufanya biashara
na ninyi. Tumelisema hilo siku nyngi, lakini MUNGU alisubiri tufike hapa
tulipofika.
+ Juzi nilipata neema ya kuangalia matokeo
ya toba, niliona waziri wa viwanda wa Urusi alikuja na ujumbe hapa akitafuta
mahali pa kuwekeza, nikajua kumekucha hapa! Sijawahi kusikia lile taifa la
Urusi linakuja hapa kuwekeza. Kwa hiyo kwenye lile shamba lako la Bagamoyo
ujiandae wanakuja.
Isa.60
- Mataifa ya Kaskazini yataanza lini kuja kulitafuta Kanisa?
+ Wengi tumetafuta kuona Isa.60 itatokea lini; yaani kaskazini
kuja kulitafuta Kanisa; kuja kutafuta biashara huku!
Lakini sasa huyu aliyeyatamka hayo, huyu
aliyeandika haya, sasa hivi yupo.
+ Sasa ninyi kosa mnalofanya mara nyingi,
ni kumtafuta kwa macho haya. Mkimkosa mnaanza, yuko wapi sasa, amevaa suti
gani?. Siyo hivyo! Wewe amini tu
yupo hapa madhabahuni!
Na siyo tu hapa, yuko ndani ya moyo wako.
Na siyo tu ndani ya moyo wako, bali yuko kwenye kila kitu kinachoitwa kwa jina
lako.
+ Sasa hivi mahali popote ulipo, unatakiwa
useme “wewe MUNGU uliyetuma wote vizazi
vyote, wewe uliyemtuma MUSA, ukamtuma Yoshua, ukamtuma Eliya Mtishbi, ukamtuma
Elisha, ukamtuma YESU, ukamtuma Paulo, ukamtuma Petro, ukamtuma Tito, ukamtuma
Timoteo, ukamtuma Eliya Kizazi cha Nne, nimeambiwa uko hapa, nataka nikuone
sasa hivi!” “Nimeambiwa sasa hivi
hujatuma tena mwingine, bali uko wewe mwenyewe!! Nataka nikuone kazini kwangu,
nikuone kwenye biashara yangu!”
+ MUNGU awape neema ya kuona haya na
kuyatendea kazi. Huu si wakati tena wa ku-“struggle” (kuhangaika) na
kubahatisha! Tunaishi na yeye aliyetuma wote vizazi vyote. Hiki ndicho kipindi
cha kuwaona wafanyabiashara wa kutisha kutoka ndani ya Kanisa.
Isa.65:16
+ Wakati naanza ibada hii nilianza na Isa.65:16 kwamba ndiyo majira yake,
kwamba kila anayeapa sasa hivi aape kwa MUNGU wa kweli, kila anayefanikiwa
lazima afanikiwe kwa MUNGU wa kweli, ndiyo kipindi hiki, siyo kesho!
Imekwishafika! Siyo kipindi tena cha kuishi kwa wasiwasi, kwa mashaka na hofu!
Siyo kipindi cha kusema nakufa kesho, nakufa keshokutwa. Hapana!
Mpango wa kufa haupo tena. Tuna mpango wa
kuishi na kufanya mambo makubwa sasa hivi. Tuna mpango wa kupanda miti ya aina
ya mipingo, inayokomaa baada ya miaka 90+.
Hag.2:7-9
– Hiyo Nyumba ya BWANA yenye utukufu kuliko vizazi vilivyopita ni lini
itajengeka?
+ Kwa
kweli kulikuwa na maswali mengi pamoja na
Hag.2:8 inayosema kwamba dhahabu zote na fedha ni mali yake. Sasa wengi
walikuwa wanasema, mbona naishiwa, mbona nakosa hata vazi la kuvaa, mbona
nakosa mtaji, na wewe MUNGU nimekufuata unasema dhahabu na fedha ni zako? Kwa
kweli sasa hivi ni zake, na yupo! Ila bado anataka wewe uwe na Bureaux de
Change (duka la kubadilishana fedha) ya kwako. Nataka mtambue maswali yote,
wako wengi mna maswali kuhusu watoto, sasa mtafyatua watoto!
2. Ufuasi
wa kweli
+ Najua ninyi ni wafuasi lakini kuna
kipindi mlikuwa mnaiingiwa na wasiwasi. Kuna kipindi mlikuwa mnasema, mh, hivi
tutafika kweli! Sasa kwa kuwa maswali yote yanajibiwa, ni lazima muwe wafuasi
wa kweli.
+ Katika 1Nya.11:1-2, tunaona wazee wa Israeli wakimfuata Daudi wakisema “... sisi ni mfupa wako na nyama
zako”. “Tunasema hivyo kwa sababu, hata
kipindi Sauli alipokuwepo, wewe ndiye uliyekuwa unatutoa na kutuingiza”. Kwa
sababu hiyo tupo tayari kukufuata.
+ Sasa niwaulize
swali, “hivi kipindi Eliya yuko kwenye
viungo vya ufunuo, sikuwa nawaingiza na kuwatoa?” Sasa wasiwasi unatoka
wapi? Sasa leo niseme kama Paulo alivyosema katika 1Kor.11:1, alisema hivi
“Nifuateni mimi kama ninavyomfuata Kristo mtafika”!
+ Sasa na mimi leo nasema hivi: “Kama vile ninavyo mfuata huyu Aliyetuma
wote Vizazi vyote bila kudondosha hata neno moja, na ninyi nifuateni, mtafika”!
Wasiwasi na mashaka leo tuondoe!
+ Kuhani mmoja wa biashara ameniambia “Miak1000 unaapa mno, mpaka
unapitiliza”. Sasa nitafanyaje na ninyi mnaamini sana? Leo sina haja ya kuapa,
kwa sababu mumeshaamini. Lakini nataka niseme hivi, “ni lazima tufike”! Kufika, ni lazima, na kufanikiwa ni
lazima.
Hatua za kuchukua
(i) Ebr.6:12 – Mwamini aliyesimama mbele
yako au
Aliyepakwa Mafuta kuwa ana kitu cha Ziada.
Neno linasema kuwa “msiwe wavivu wa kuwa wafuasi wa wale waliorithi ahadi za MUNGU kwa
uvumilivu”! Hivyo usiwe mvivu wa kuwa mfuasi; usiwe na mashaka wala
wasiwasi. (ii) Ukubali kuachana na mambo yote ya zamani, Mt.4:18-22, ili uyafuate haya ambayo MUNGU anakuelekeza.
(iii) Ni
vizuri kutangaza hadharani kwamba unamfuata nani (1fal.19:19).
(iv) Ukubali
kuingia agano la kuwa kama mtoto, usiwe mtoto, bali uwe kama mtoto (Mt.18:1-4). Ukiwa mtoto watakuwekea
agano la kutokua. Lakini ukiwa kama mtoto maana yake:
(a) Unakubali
kuonywa Meth.3:12.
(b) Unakubali
kutenda kama
Baba anavyotenda
(Mwa.28:16-22).
(c) Unakubali
kutetea maono (2Fal.2:3,5) kama vile
tunavyomuona Elisha Kizazi cha Pili walipomkatisha tamaa, alisema nyamazeni
mimi najua.
(v) Ukubali
kurarua mavazi yote ya zamani (2Fal.2:9-12).
3. Utawala wa amani
- Zab.99:1-2
+ Neno linasema “BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;
ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.”
“BWANA katika Sayuni ni mkuu, naye ametukuka juu ya mataifa yote.” Kwa
kuwa BWANA ametamalaki, lazima amani iwepo.
+ Kwenye familia yako lazima amani iwepo;
+ Kwenye agano lako lazima amnai
iwepo; + Kwenye kazi yako lazima amani iwepo; n.k.
Maana yeye ndiye BWANA wa amani.
Isa.2:4 imetimia
+ Msitari huu unasema kuwa “Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi,
atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki
yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala
hawatajifunza viata tena kamwe”! Kwa sababu BWANA sasa ametamalaki ni
wakati wa amani. Hii ni thamani na faida ya kuishi mahali ambapo huyu MUNGU Aliyetuma wote vizazi vyote
ambaye tumemkabidhi kila kitu ili atamalaki.
+ Nataka uone pale nyumbani kwako MUNGU
ametamalaki; pale kazini kwako au ofisini kwako nataka uone MUNGU ametamalaki.
Akitamalaki lazima amani iwepo na unachokitaka lazima
upokee.
Kama amani inatawala lazima ianzie moyoni mwako:
+ Usiishi maisha ya kushtuka-shituka tena;
+ Usiishi maisha ya hofu tena;
+ Usiishi maisha ya wasiwasi tena;
+ Usiishi maisha ya kuona kuwa unakufa “anytime”.
4. Mwa.8:4 – Kanisa
kwenda juu
+ Neno linasema “Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, Safina ikatua juu ya
milima ya Ararati.” Katika 1Fal.8:2,
neno linasema “Wakakutana mbele ya
mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukukuu, katika mwezi wa
Ethanimu, ndiyo mwezi wa saba.”
Safina maana yake ni Kanisa, kwa hiyo
Kanisa limetoka chini limekwenda juu. Kwa hiyo wewe hapo ulipo umetoka chini
umekwenda juu kwa uhalisia kabisa. Kwa hiyo, katika mwezi huu lazima ujisikie
kwamba yule MUNGU Aliyetuma wote vizazi vyote, unatembea naye kila mahali.
+
Kumb.28:13 mstari huu unasema “...
utakuwa juu tu, wala hutakuwa chini”. Huko nyuma “graph” ilikuwa inapanda
na kushuka, lakini sasa hivi, kwa kuwa unaishi kwa huyu Aliyetuma wote,
hutashuka tena. Katika kila unalofanya utakuwa juu tu.
+ Kanisa lilikandamizwa miaka mingi,
lakini baada ya MUNGU Aliyetuma wote Vizazi vyote kukabidhiwa kila kitu, sasa
Ameleki hawatalizuia tena milele.
5. Katika Vizazi vyote wenye haki walipata shida sana, na hasa wale
viongozi waliokuwa wanajenga msingi, na waliokuwa wanajenga jengo.
+
Katika Vizazi vyote Kanisa lilifunuliwa Viongozi wakiwa wamekufa (yaani Kanisa
lilifunuliwa baada ya viongozi wa vizazi kufa), sasa hivi limefunuliwa na
Aliyetuma wote Vizazi vyote, Kiongozi na anaofuatana nao tukiwa hai. Sasa kwa
kuwa tumefika kwenye kituo hiki cha huyu MUNGU Aliyetuma wote, ina maana hata
anayejenga jengo hafi na wewe hufi! Agano lako halitakufa. + Kizazi cha Kwanza
mpaka cha Tatu, yule anayejenga jengo alipokufa na Kizazi kilikuwa kinakufa. Yos.23, alipofikia hatua ya kulala na
kizazi cha kwanza kikaishia hapo. Elisha alipofikia hatua ya kulala na Kizazi
cha Pili kikaishia hapo. Akina Petro, paulo, Tito na Timoteo walioachiwa Kizazi
cha Tatu kujenga jengo, walipolala, Kizazi cha Tatu nacho kikalala.
+ Sasa Kizazi hiki cha Nne ni Kizazi cha
mwisho, ni Kizazi ambacho lazima kimilikiwe na MUNGU mwenyewe, mimi sifi na
wewe hufi. Hii inatokana na kwamba
tumefika kwenye kituo hiki cha MUNGU Aliyetuma wote vizazi vyote. Hivyo
mshukuru MUNGU hata vitu vyako vizuri havifi tena; ule wasiwasi, mashaka na
hofu uache. Tumefika pazuri kwa Damu ya MUNGU Mwenyewe.
No comments:
Post a Comment