MIAKA1000 ELIYA
KIONGOZI WA MAKUHANI KIZAZI CHA NNE
9 ELULI 4
9 ELULI 4
UFUNGUO
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya siku ya pili ya ufahamu wa Kanisa na macho ya kuona kama
MUNGU.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya mbegu ya rohoni ambayo MUNGU amekwisha kuirejesha ndani ya Kanisa.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa sababu jengo linaonekana wazi wazi 1Kor.3:9
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya shamba limekuwa safi kwa sababu kisiki kimeondolewa, moyo
mbaya ulikuwa ndani ya shamba umeondolewa kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya utawala wa Kristo kurejeshwa na bila nguvu ya utawala wa Kristo
tusingefika mahali hapa.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya ufufuo wa kwanza ambao umerejesha kila kitu na tumepata
mahali pa kusimama na kurejesha kila kitu.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya majeshi ya Eliya
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya Mnara wa Neno ambao umefuta minara ya maneno na bila Mnara
wa Neno tusingefika mahali pa shamba.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya Mnara wa Eliya umeangusha minara yote ya adui.
= Tumshukuru
MUNGU kwa ajii ya madhabahu ya utukufu wa Kanisa na imekwisha kusimama.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya madhabahu ya umilele na kupitia umilele mbegu ya rohoni
imeonekana.
= Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya jengo la MUNGU limeonekana wazi wazi
= Kutubu
kwa chochote kinachoharibu Ufalme wa MUNGU.
MSINGI
Tumeanza
siku saba za kupanda mbegu ya rohoni.
KUHANI KIONGOZI : MIAKA 1000 YA KUTAWALA NA KRISTO. |
Jana
tumeondoa mahali pa chako, chetu, chao na changu.
MUNGU
jana amefuta roho ya kutokuamini Lk.1:18
nitajuaje neno hili na mimi ni mzee…..
Zakaria
aliambiwa atapata mtoto hiyo ni mbegu tayari ilikwisha ota rohoni. Mbegu ya
mtoto ilikwisha pandwa rohoni lakini kisiki kiko ndani ya shamba la Zekaria
kisiki kilikuwa itakuwaje neno hili na mimi ni mzee na mke wangu ni mzee na
kipindi kilichopita kilikuwa ni kisiki kingine, kulikuwa na magugu ya umri
yalikwepo yameoteana ili kuzuia lile neno ambalo MUNGU alisema naye kupitia
malaika. Kisiki kingine ni kutokumuamini malaika.
Kisiki
litakuwaje neno hili lilikuwa pia kwa mariam saa malaika anakuja na kupanda mbegu
ndani ya mariamu akasema litakuwaje neno hili. Wakati malaika anaenda kwa mariam
tayari mbegu ilikuwa ndani yake, tazama kisiki kilichokuwa kwa mariamu ni
kuangalia mazingira.
·
Itakuwaje umri ni mkubwa sana.
·
Itakuwaje mazingira niliyokuwa nayo.
·
Itakuwaje maisha niliyokuwa nayo.
·
Ni shida sana inayosababisha mbegu isiote.
·
Jana MUNGU ameng’oa mashina yake na mizizi.
Tunamshukuru
sana MUNGU kwa kutukumbusha hii mbegu ya rohoni ambayo tunaendelea nayo siku
saba.
MWANZO WA SOMO
A. PANDA MBEGU YA ROHONI KWENYE SHAMBA LA MUNGU SIO LA MIAKA1000 (MATH.16:18)
ELIYA AD2 MUNGU WA MAJESHI KRISRO KIZAZI CHA NNE |
Ukipanda
mbegu ambayo ndani yake kuna wadudu haioti.
Miaka1000
anatamani tufike mbinguni na yeye ni Neno peke yake ndilo analolitaka. Kulingana
na MUNGU anavyosema na wewe utoe sawa sawa. Miaka1000 anaomba tuwe na amani
kabisa tutafika tu. MUNGU atakaposema na wewe kwa ajili ya kutoa utoe hata
milioni moja itaota kwa sababu shamba ni la MUNGU, tusiwe na maswali ni mwisho.
Na ndiyo msingi tuliyojengewa na Kristo chochote kinachotamkwa hapa madhabahuni
ni cha MUNGU mwenyewe.
B. TUNZA MBEGU YA ROHONI SIO YA MWILINI
Wengi
tunapenda na tunao uwezo wa kutunza mbegu ya mwilini lakini ya rohoni hatuwezi.
Wengi
kilichotokea miaka 60 unakikumbuka lakini ulichofundishwa juzi hukumbuki. Tunatakiwa
kutunza mbegu kuliko tunavyotunza nyumba zetu, gari letu na mali zetu. Kutunza
mbegu maana yake usiwe mlalamishi, mlalamikaji na kile kitendo cha kusema
tumepanda sana lakini hatujawahi kupata sana.
Jinsi
ambavyo tulikuwa tunakiri kutunza mbegu ya mwilini leo tuwe zaidi kwa habari ya
mbegu ya rohoni, Neno tunaloambiwa tulikamate kuliko kitu chochote. Kuanzia
sasa hivi hii mbegu tunayopanda rohoni tusipalilie kwa kunung’unika, kusingizia
na kuseng’enya hapo ndipo MUNGU utaona ana chipusha ule mti uliko kwenye kitabu
Ez.47:12/Ufu.22:1-2
Eze.47:12
Na karibu na mto karibu na
ukingo wake upande huu na upande huu……….
Neno
uliloambiwa limetoka mahali patakatifu. Afya tele kila wakati unapokuwa umetoa
mbegu na jinsi MUNGU alivyokupa.
Ufu.22:1-2
Mto
wa maji wa uzima ni Neno linalotoka madhabahu.
Umefika
wakati wa kupanda mbegu itaota na matunda yake yatamponya kila mmoja.
1. Mahali
unapopanda umepafahamu kuwa leo unapanda kwenye shamba la Bwana na hiyo mbegu mwezi
huu Eluli inaota. Unabii unasema unapanda kwa mda mfupi unavuna kwa muda mfupi.
Unapanda
mbegu inakupa kibali, kazi, shamba, nyumba, gari na kila upande bila kusita.
Kile
ambacho MUNGU amesema kwa mkono unatoa unapokea leo kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
+ Matokeo yake mwezi Eluli hiyo ndiyo akili
ya MUNGU.
MUNGU
atusamehe kwa wazo lolote lililotaka kutuibia lazima tutafaulu kwa Damu ya Haki
Kweli na Hukumu. Matunda yatakayopatikana ni shamba, mtaji, nyumba, kazi,
biashara.
Tunamshukuru
MUNGU kwa ajili ya kupanda kama MUNGU na tumepanda kwenye shamba lile
alilopanda yeye na kuamini kila mwezi linazaa matunda.
Kuna
mti wa matunda yanapatikana kila wiki walichukua hapa. Sasa kila wiki matunda
lazima yapatikane.
+ Shamba sasa tunapanda mbegu ya rohoni.
Tunamshukuru
MUNGU mbegu tuliyopanda lazima iote na ikiota lazima izae na lazima tupeleke
sokoni na lazima inunuliwe.
Matunda
ya Southafrica na matunda ya Lushoto ya nje ya nanunuliwa na ya Lushoto
hayanunuliwa wakati yote ni matunda yanayofanana ni kwa sababu hiyo mbegu ya
rohoni imeibiwa.
Utasoma
neema kubwa wamefanikiwa Mlima wa Maono lakini ukienda Uganda itakuwa hivyo
hivyo. Siloam inafunguliwa Denmark itakuwa hivyo hivyo kwa sababu mbegu
imerejea Kanisani.
Miaka1000
anasema anaomba umwambie MUNGU nakushukuru kwa ile mbegu iliyolikuwa imeibiwa
rohoni ambayo ilisababisha ni kipanda kitu hakioti lakini sasa imerejea nikipanda
kitu kinaota.
Aliyekuja
jana anafanikiwa lakini wewe hufanikiwi kwa sababu unawaza jinsi
wanavokukanyanga inasababisha usifanikiwe au usipokee. Lakini yeye aliyekuja
muda mfupi anayochojua ni Neno tu ndiyo maana anafanikiwa, na wewe usiwe mikono
nyuma toa katika shamba la MUNGU.
Tumepanda
mbegu inaota na matunda yanaonekana na tutapeleka sokoni. Sasa hivi usiwe na haraka ila uatamie kwa majira ya MUNGU itazaa
na MUNGU yupo na nchi ipo kila kitu kizuri kinaendelea kuzaliwa.
Siku
ya sita kila kitu nilichopanda ni chema sana.
Ikifika
siku ya saba tutaandika nne na kusema lazima nipate, kama ni nyumba, shamba, mtoto,
gari na jana tulifuta changu chako, chao na chetu, tuliua ubinafsi kabisa.
Mbegu
imeshapandwa tayari umekwisha kupanda mbegu rohoni. Mambo mengi MUNGU ameyaweka
ndani yako. Kabla ya mbegu ya rohoni ilibidi kwanza umilele urejee rohoni.
Usifikiri
kwamba utaanzisha shamba, biashara na kiwanda kwa upya. Hii mbegu tunayopanda
sio inayokwenda kuanzisha kuumbwa kwa mtoto. Lakini tunao umilele na MUNGU
amepanda ndani ya nafsi yako na moyo wako.
Tunamshukuru
MUNGU kwa uongozi wa MUNGU kila kitu kinafuatana na sisi. Kama hatukurejeshewa
umilele kusingekuwa na kitu ndani yetu.
Kabla
ya kupanda mbegu kisiki kiliondolewa kwanza na magugu, moyo mchafu na ndipo
ikaja mbegu nzuri.
Unaposikia
Kiongozi wa Makuhani akisema hiki kitu ni halisi na sisi tunasema ni halisi
kweli. Kufuatana na masomo yanayoendelea
ni kitu halisi kabisa ndiyo maana MUNGU amekuja kwa mfano kabisa ili
tusikosee kwa sababu hii mbegu ya rohoni tunayopanda ni lazima itokee kwa
uhalisi wake.
Asubuhi
tumefuta hii mbegu ya kusita kusita, kumbe kulikuwa na maswali yaliyokuwa
yamejaa ndani ya mioyo ya wakamilifu ndio yaliyokuwa yanasababisha mikono ikae
nyuma na kufunga mikono lakini MUNGU amefuta kwa Damu ya Haki Ukweli na Hukumu.
Kile
kitu MUNGU amekusudia kukupa tayari kimeshatokea na sio MUNGU anataka kupata
pesa yako ila anataka moyo wako. MUNGU anachoangalia ni moyo wako peke yake na MUNGU
anataka kukujaribu ili aangalie kama utamtolea kwa uaminifu.
Ndipo
alipomjaribu Ibrahimu akamwambia amtoe mtoto wake. MUNGU ameangalia ule moyo wa
Ibrahimu akamwambia kwa kuwa umekuwa na moyo mwema lazima nikubariki. Hiyo
sadaka itakwenda kutibua maji ili vitu vitokee. Ndiyo yule malaika atatibua ili
vitokee na itakwenda kuchemsha ili vile vitu vitokee kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
Mwa.22:3-17
Ibrahimu alitoka na
mwane…….
Ibrahimu
hukumzulia MUNGU kumtolea sadaka lakini sisi Kiongozi wa Makuhani alituona tunamzuilia
MUNGU kwa kuweka mikono nyuma.
Yule
mwanakondoo asingetokea ameinua kisu amkate Isaka hapa ndiyo dunia na ulimwengu
waliibia hapa kutoa sadaka zao. Roho ya utoaji waliiba hao na dunia hawaogopi
kutoa sadaka.
Wengine
wakaiba vibaya wakaanza kuchinja watoto na wake zao. Sadaka ni ile inayomgusa MUNGU,
ili isababishe MUNGU asimame na aape kwa ajili yetu kwamba atatubariki.
15malakika wa bwana wakamwita
ibrahimu…..
Si
mchezo MUNGU kusimama kwa ajili yako na kusema huyu jamaa atazaa kuliko mataifa
yote na kilichosababisa MUNGU aape ni sadaka.
MUNGU
amepanda ndani yako ila unatakiwa upande sadaka ili itokeze nje.
1Fal.3:4-7
Lakini
baada ya kutetekeza sadaka elfu kwa maelfu maana yake ni sadaka maelfu na
maelfu kama ni ng’ombe ni maelfu elfu. Wala si baada ya maombi ya hatari au
shukrani au power ni baada ya kuteketeza sadaka wala si kuja Kanisani. Ni baada
ya kutoa sadaka ya kuteketezwa MUNGU akatokea saa ile ile (alimwambia omba
lolote nikutendee).
Ibrahimu
akatoa tena sadaka na MUNGU akaapa tena kuwa atambariki kwa kuwa na mali kuliko
wote, fedha kuliko wote na vikatokea wazi wazi. MUNGU anafanya vitu visivyokuwa
ya kawaida lakini MUNGU anataka tupande sadaka nzuri. Hakuna mahali MUNGU
alisema ajaribiwe ni kwenye sadaka tu. Kwa sadaka zisizokuwa za kawaida, utoaji
usio kuwa wa kawaida kama kichaa unaleta sadaka isiyokuwa ya kawaida.
Sisi
tumepewa utajiri mkubwa zaidi kuliko wa Sulemani.
Siku
moja nilikuwa na wafundisha Makuhani utajiri sio zile fedha za kula. Sio gari
la kwenda Kanisani na sio nyumba yangu. Kama kipato chako kwa siku ni milioni
kumi bado wewe ni lofa, kama kipato chako ni hazina hamsini, hazina mia wewe ni
lofa. Angalau yule tunaweza kusema ni tajiri anaanzia bilioni moja kwa siku
huyo ndiye ni mjasiria mali. MUNGU anakwenda kutuinua na ni lazima.
Ukianza
kwa bilioni moja kwa siku, kwa mwezi unaweza kuwa na trilioni moja ndio unaweza
kuita raisi wa Marekani na kula naye chakula na kumuuliza nasikia kwenye jimbo
lako linashida nitashughulika nalo. Ni mahali tunatakiwa tufike zaidi ya
utajiri wa Sulemani na tunatakiwa kupanda mbegu nzuri ya rohoni ili mataifa
waje.
No comments:
Post a Comment