MAJIRA NA NYAKATI

MAJIRA NA NYAKATI YA SIKU YA LEO.
Siku ya NNE.
Lango la 25.
Mwezi ABIBU.
Mwaka wa 6 wa UKAMILIFU NA UTIMILIFU WA ISAYA 2:2-4 NA ISAYA 60.
(29 October 2016)
MAREJESHO YA SHAMBA LA FEDHA NA DHAHABU ROHONI KIZAZI CHA NNE

MIAKA1000 ELIYA
KIONGOZI WA MAKUHANI KIZAZI CHA NNE
10 ELULI 4
UFUNGUO
=     Tunamshukuru MUNGU kwa ajili ya siku ya tatu ya faida na thamani ndani ya mwezi Eluli mwezi wa kufanya mambo makubwa na kumaliza kwa muda mfupi.
=     Kama huna mbegu ya rohoni huwezi kuwa na thamani na faida.
=     Tunamshukuru MUNGU mbegu ya thamani na faida imefunuliwa rohoni.
Mwa.2:2-4
=     Kila unachofanya sasa kinathibitika wazi wazi.
=     Tunayo mbegu ya rohoni na tunalo shamba liko tayari kupandwa, kupaliliwa na lina beacon nne, majira, hakikazi hadi milele, mafuta 7 ya ukamilifu ya siku ya 1-7 na ni mafuta ya kutukamilisha ndani, damu kamilifu ambayo ni beacon nne linalozunguka hilo shamba. Kuna beacon ya ule upanga ulikuwa ukilinda Bustani ya Eden, liko jiwe likizunguka hilo shamba, tunayo majeshi ya ufalme wa MUNGU wa Eliya likizunguka hilo shamba, ufufuo wa kwanza unazunguka hilo shamba la rohoni, tunayo sadaka ya amani inayoongoza Kanisa, madhabahu ya utukufu wa Kanisa ambayo imekwisha kusimama vyote viko ndani ya shamba na tunayo hakika na shamba ni zuri na linaleta matunda.

Esta.3,4,5
=     Esta ilibidi aandae karamu ya kumwangamiza Hamani yeyote aliyeinukia Israel. Hamani alikuwa adui wa Israel na alikwenda kunyongwa.
=     Aliyepanga jambo lolote baya anakwenda kutundikwa kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
=     Adui yeyote aliyepanda jambo baya kwa ajili yako amefutwa.
=     Kuuza watoto, mke na kuzuia vitu vyako sawa sawa walivyotengeneza watakuwa wamejitengenezea wao wenyewe.
=     Karamu tunayokwenda kushiriki leo Hamani yeyote anakwenda kutundikwa kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
=     Hamani yeyote aliyetengeneza kesi yeyote mbaya, kufanya makafara kwa ajili yako anakwenda kutundukwa kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
=     Kitu chochote wanachotengeneza adui yako ukikirudisha kinakwenda kuwaangamiza moja kwa moja
=     Silaha zina macho na zinaenda moja kwa moja ndiye ule mti wa matawi hamsini.
=     Waliokutengenezea kesi, hukumu, aibu, makafara, waliokupiga power chafu leo tunakusanya tanakwenda moja kwa moja na kuwaangamiza wao.
=     Wangejua wasingetengeneza na leo wanaangamia moja kwa moja.

MSINGI
Jana tuliona MUNGU akitukumbusha mbegu gani ipandwe rohoni ni ili mbegu ya thamani na faida ionekane. Kitu cha peke unatakiwa upande ni cha thamani, kama ukipanda mahindi yanaota, ulikuwa unatafuta mbegu nzuri Mwa.22:1-17 Ibrahimu alipanda mbegu nzuri ilibidi amtoe mwanae Isaka huyo ndiye aliyeenda akampanda ndio iliyosababisha MUNGU atokee. Mahali MUNGU anakutokea ili akubariki ni mahali pa mbegu ile ya kuteketeza sadaka nzuri ya thamani.

Kuna aina mbili anatokea ni:
1.  Sifa zinazomgusa MUNGU
2.  Mahali MUNGU anatokeza ni mahali pa sadaka nzuri.



MWANZO WA SOMO
ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI
Kristo Kizazi Cha Nne.
Tunachukua alichofanya Ibrahimu tukiingize rohoni.
Kila alichofanya MUNGU ile mbegu aliyopanda ikaonekana walichukua.

+     Mjini wakitaka kuwa matajiri lazima watoe mke na mtoto wake.

Zile sadaka zote ulizotoa kwenye dini na dhehebu leo tunaenda kuzichukua rohoni na kuzileta hapa.

·        Kizazi cha 1 fedha unaziona Kanisani.
·        Kizazi cha 2 fedha unaziona Kanisani.
·        Kizazi cha 3-4 hazionekani Kanisani.
·        Zilipotelea kwenye bonde la uvuli wa mauti.
·        Ibrahim alipanda mwilini.
·        Yusufu alipanda mwilini.
·        Sulemani alipanda mwilini.
·        Paulo mwenyewe aliwakabidhi wazungu
·        Tunachukua Isaka tuliyomtoa mwilini tunamleta rohoni.

Lazima utawaona singa singa wanakuja Kanisani kwa sababu fedha zote zimehamia Kanisani.

+     Unakumbuka kuna shimo lisilovukika rohoni na mwilini.

Sisi tumehamia rohoni kwa uhalisi kabisa na fedha lazima tuchukue rohoni.

Hagai:2:8-9
Ingawa utaona fedha picha yake ni ya mtu na mwanadamu lakini sasa hivi lazima iwe picha ya MUNGU mwenyewe.

Shimo lisilovukika kwa kupitia Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga lazima fedha na dhahabu zirejeshwe Kanisani.

Kut.10:24-
Farao akamwita Musa…….
Leo hata senti moja haibaki mwilini hata kipande kimoja cha dhahabu hakibaki mwilini. utapita dini yeyote au dhehebu iliyopitia unapita rohoni na kuchukua fedha zote na dhahabu zote.
Hata kama uliwahi kutoa rushwa fedha zinarejea rohoni.

Kujenga madhahabu ya hilo shamba la fedha na dhahabu rohoni kizazi hiki ili zipate mahali pa kukaa rohoni.

·        Paulo alikabidhi fedha zote kwa waovu.
·        Sulemani alikabidhi fedha kupitia uzinzi.

Tunatubu kwa sababu Kuhani Kiongozi alisema atasimama na Neno la ufunuo tu.

Tusamehe kwa ajili ya fedha tulizotoa kwenye dini na dhehebu ambazo zilikuwa zinaiba fedha tunazoendelea kutoa sasa.

Ufu.11:6
+     Kubadilisha maji kuwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

Tuna hii damu ya kubadilisha fedha na dhabahu zilizokuwa mwilini na kurejesha rohoni.

Tunamshukuru MUNGU kwa kuturejeshea shamba la fedha na dhahabu rohoni kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu. Kuanzia leo vitu vyote vilivyokuwa mwilini vinarejea rohoni.

Mwa.17:1-6
Abrahamu alipokuwa mtu wa miaka 90………
+     Leo nataka uone kuna jambo la zaidi liko hapo.

Ukienda pale mjini ilikuwa hoteli ya Sheraton sasa hivi inaitwa Serena na ile nyingine ya zamani Kilimanjaro sasa hivi inaitwa Hyatt kwa sababu wanataka kukwepa kulipa madeni ambayo wanadaiwa.

Kama leo naitwa Jambo Jipya nikaenda kwa mwanasheria nikabadilisha nikaitwa Toba ya kweli mimi sidaiwi lile deni tena.

MUNGU alimwambia agano hili nitalifanya kuwa imara na mataifa wote watatoka kwako. Unaweza kwenda kariakoo utakuta leo anauza mavazi kesho anauza vinyago base yao ilikuwa hapo. Nguvu waliyokuwa wanatumia kubadilisha jina ilikuwa ya Ibrahimu.

Nataka leo ujue hiyo nguvu ambayo ndio hasa tuirithi kupitia kiuno cha Eliya leo tuchukue moja kwa moja. Tulishafundishwa kila ambacho MUNGU amekitoa walikichukua na kukiwekea agano la damu za wanyama na ndege kwa ajili ya ulinzi.

·        Shamba la rohoni linalochukua fedha mwilini na kurejesha rohoni.
·        Uzao mwingi maana yake kupata faida nyingi

Wafalme sio lazima awe anayetawala ila kama unaongoza sekta ndio ufalme. Utakuwa mkamilifu mwenye biashara kubwa, kiwanda kikubwa au mwenye supermarket kubwa ilikuwa sio rahisi.

1.  Gal.3:29
Ikiwa ninyi ni Wakristo mmekuwa uzao wa Ibrahimu sawa sawa na ahadi….
Anayetakiwa kurithi hiyo nguvu ya Ibrahimu kupitia Kristo ilikuwa ni lazima kwanza kupanda mbegu hii ya rohoni.

Tunamshukuru MUNGU kwa habari ya marejesho ya shamba la dhahabu rohoni na hii mbegu tunapanda rohoni. Hili shamba la MUNGU ambalo tunapanda ndani yake na kuna plot nyingi plot mojawapo ni fedha na dhahabu.

2.  Mwa.22:1-17
Ikawa baada ya mambo haya MUNGU alimpa mtihani (maana anayempa majaribu mtu ni shetani) Ibrahimu……
Sasa hivi ni wakati wa uhalisi wa kutoa sadaka kubwa ya kukuuma na waliokuwa wanafanya hivyo ni dunia. Kuna nabii wa uongo mmoja yuko hapa mjini akiteremka kwenye gari kuna wakina dada ambao wanampepea.

Waliomchukua Isaka ni wale waliokuwa wanasema lete jogoo. Ukiwakuta mjini wanaendesha magari makubwa kumbe wametoa jogoo au mtetea maana yake baba na mama. Kwa kweli dunia haifai ilikuwa mwilini kweli kweli. Leo fedha zote mwilini tumechukua, watoe jogoo wasitoe jogoo hawapati fedha mpaka waje Kanisani na hivyo wao wameshasikia. Na kama uamini nenda kwa mganga sasa hivi watakuambia leo mambo yameharibika ndiyo utaamini kwamba hapa yuko MUNGU mwenyewe. Neno linalotamkwa hapa sio la kubahatisha ni la MUNGU mwenywe. Kule mjini ni biblia lakini hapa ni kitabu cha Neno la MUNGU cha haki kweli na hukumu, kule mjini wanasema ukweli na hapa tuna sema kweli.
Fedha zitabaki hapa kwa wanaomwabudu MUNGU kwa roho na kweli. Ndio maana tulikuwa tunashindwa kutoa fungu la kumi kwa sababu waovu walikuwa wanamtoa Isaka. Machimbo sasa hivi yamehamia Kanisani na kukuambia hivyo ni kweli kabisa. Leo ile nguvu ya kutenda Neno tumeichukua na Neno kuwa mwilini ni mwisho.

3.  Mwa.26:12-
Isaka akapanda mbegu katika nchi ile akapata vipimo mia….
Kumbe unapokuwa na biashara inaanza jamaa wanakuja usiku wanafukia. Amaleki Kut.17:1- ni mpinzani kwa mwenye haki wakiona umeinuliwa wanakufukuza sokoni. Kila aiyeokoka akianzisha biashara pale Tegeta ninatoa mfano wa pale Tegeta kwa sababu waliokoka wakifungua biashara wanapandishiwa bei ya pango hii ilipitia kwa Isaka alipokuwa anachimba kisima walikuwa wanamfukuza.

Si tu kwamba fedha ulizokuwa nazo hata fedha ulizoacha kule mwilini tunachukua leo. Kwa hiyo kinachosababisha tubarikiwe ni agano la MUNGU aliingia na Eliya wa kizazi cha nne. Walipogundua kwamba kule alikokwenda Isaka alifanikiwa kwa kuchimba kisima wakamfuata kule sasa utaona wanakuja hapa sisi hatujaona maji bali tumepata maji, leo tumeshinda.

Huko nyuma ukianzisha biashara kama hukutaka kuwa mwilini walikuwa wanakufukuza. Walikuwa na vikao vyao nuruni wanakutunza rohoni mpaka unakubaliana nao kuwa upande wao.

4.  Mwa.31:17-
Ndipo Yakobo akawapandisha wanawe na wake zake……
Sasa wewe usiondoke na vinyago vya baba yako tunaondoka na fedha na dhahabu tu. Kumbe ilikuwa ni lazima watufuate kwa sababu walikuwa na siku 7 yaani ukichomoka tu lazima mizimu ikufuate, Yakobo alipotoka ambaye ni Israel alifuatwa na Labani. Ulikuwa umeokoka walikuwa wanakufuatilia mpaka urudi kwa sababu ya agano hili lakini leo tumetoka moja kwa moja hutarudi tena kwenye kanuni za zamani.

Hata Labani akikufuatia hawezi tena kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu. Dhambi ulizokuwa unafanya zamani zikikufuatilia hazikuwezi tena kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

Washami 1Fal.20:23-27 Basi watumwa wake mfalme wa Mshami…
Wakiona umeshindikana watatafuta mazingira ya kutengeneza mpaka ushuke moyo. Yaani wewe uko juu wanatafuta Neno la kukushusha ukishuka tu watakuangamiza. Watakutukana ukikasirika wanakomboa kila kitu. Nyie mnaokasirika kasiria, mnaochukia, nyie wenye Phd ya kukasirika haya. Kazi ya Mshami ni kukushusha moyo, na kama mwengine hawana Phd basi wanayo masters ya kukasirika.

Ndio maana Labani alimfuatilia Yakobo ili awarudishe wale ng’ombe wote wa maraka raka. Wengine wanapenda kila Neno unajibu tu ili wajue kuwa unajua kujitetea kama Adamu na Hawa, tumerejeshewa fedha na dhahabu MUNGU akupe kutunza.

Washami wapo watafuatalia waone zinaenda wapi uwache kukasirika kasirika. Tulishafundishwa hapa kuinua Mnara wa Neno na kushusha mnara wa maneno. Je kuna kupendwa zaidi ya kubadilisha maji kuwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

Mnapatikana kwa vitu vidogo sana MUNGU anakupa Neno zuri eti kwa sababu ndugu hawajakupa neno zuri unakasirika. MUNGU anakulinda lakini mpaka ulindwe na security. Kazi ya mshami ni kukushusha ili kurudisha vitu alivyochukua, hata senti moja hairudi duniani. Yaani hapa Yakobo anatetea madhababu ya Israeli isingejengwa na sisi tusingeweza kujenga madhababu yote haya tunarudisha rohoni.

5.  Mwa.47:14-
Yusufu akazileta fedha zote kwa Farao hapo ni mwilini.
Ni kweli Yusufu ni mtoto wa mwisho na anawakilisha Kanisa la Israel alikusanyia Misri lakini leo tunarudisha rohoni. Shamba la fedha limesimama rohoni kupitia siku 7 hutapungukiwa tena, hutakuwa hohe hahe, ule mtaji ulikuwa unahitaji umepokea tayari.

+ Kilichobaki ni wewe kuamini tu.

Leo MUNGU akupe neema haya tunayotamka yametokea kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

6.  1Fal.3:15-
Haya yalikuja kutokea 1Fal.4:21- Sulemani akatawala katika falme zote……
Sulemani hakuwa na upungufu wowote lakini alikuwa mwilini.
Alikuwa mtaalumu wa forest kuliko yeyote.

Sasa ukija hapa 1Fal.5:1-12 hapo Sulemani alikwamia aliingia mkataba na dunia bila kujijua haya yote yalichukuliwa lakini leo tumeuvunja.

12Bwana akampa hekima…
Mfalme wa tiro ni kerubi mwenyewe.

1Fal.10:14 - unakuta habari ya Sulemani lakini mwilini.
Nataka ujue kuwa fedha zikiwa mfukoni ujue zimetoka wapi.
666 alikuwa ametawala vizazi vyote vitatu.
Dunia ndio walichukua huu utajiri wote aliyokuwa nao Sulemani, na Sulemani alikosea MUNGU alienda kuoa mahali ambapo alikatazwa kuoa na ndipo hapo fedha kizazi cha pili hazikuvuka kwenda kizazi cha tatu ndipo hapo Yesu alipowatuma wanafunzi wake kuvua samaki na kupata fedha  hapo ndipo fedha hazikuonekana tena kizazi cha tatu lakini kizazi cha nne ni kwa neema ya Eliya wa kizazi cha nne. Lakini sasa fedha zilizoishia hapo zinachukuliwa zinarejea Kanisani.

Kwa sababu tuko kwenye levo ya juu kupanda fedha rohoni ni lazima. Lakini hakikisha unakaa rohoni sio mwilini maana walioko mwilini hawawezi kupata tena fedha. Tumezipata tunachofanya leo ni kwamba hizo fedha zilizopotelea kizazi cha 2 ndani ya Kanisa sasa zimekuja. Yaani sasa imefika tukiingia kwenye uzalishaji wale walilokuwa wanatusaidia sisi tuwasaidie wao.

Rum.2:9-10
Dhiki na shida juu ya kila mwanadamu atendaye uovu bali utukufu na heshima kwa atendae mema.

·        Myahudi kwa lugha ya kitabu anasimama kama aliyeokoka
·        Na Myunani anasimama kama asiyeokoka.
·        Kuanzia leo aliyeokoka kwanza
·        Leo Wayunani ndio wameipata leo ndio wameshikilia logos.
·        Leo fedha na dhahabu zimeondoka kwao zimekuja Kanisani.
Nataka tumshukuru MUNGU tumeshinda. Leo nenda kwenye genge lako, kazini kwako zinakuja hutaibiwa tena, ukipanda inatoa matunda lazima yaonekane hayakupukutika na hayataoza upeleke sokoni ni lazima inunuliwe.

Siloam fedha zote zinafanya kazi ya MUNGU kwa hiyo kama MUNGU amesema na wewe upande mbegu ya kueleweka upande Miaka wala Mama Siku 7 hakuna anayekula ni MUNGU mwenyewe.Kuna wengine wameanza kuwa na wasi wasi fedha iko salama inafanya kazi ya MUNGU na hakuna kilichobadilika fedha inafanya kazi ya MUNGU.

Umeanza kuuliza Miaka1000 anakuja na michango fedha zina kwenda wapi Miaka1000 anakuja na mchango kwa sababu umeanza kutoa kidogo. Kuanzi leo niwaondoe wasi wasi na hofu panda mbegu kwenye shamba la MUNGU usiogope hili ndio Kanisa ambalo hakuna msaada wa nje pia ukitoa fedha yako inafanya kazi ya MUNGU ili mbarikiwe
MIAKA 1000 YA KUTAWALA NA KRISTO.
Kuhani Kiongozi
.


Miaka1000 hasimami madhahabuni kwa ajili ya fedha anachotaka ufalme wa MUNGU uende mbele. Miaka1000 anataka mtoe ili mbarikiwe, mwende juu, fedha zote ambazo tulikuwa tumeziacha duniani tutume hii mbegu ikalete fedha zote. Kristo naye alitoa kiunua mgogo chake chote akaweka madhabahuni.

No comments:

Post a Comment