MAJIRA NA NYAKATI

MAJIRA NA NYAKATI YA SIKU YA LEO.
Siku ya NNE.
Lango la 25.
Mwezi ABIBU.
Mwaka wa 6 wa UKAMILIFU NA UTIMILIFU WA ISAYA 2:2-4 NA ISAYA 60.
(29 October 2016)
7 ELULI 4.
MAFUTA YA JENGO MOJA PEKE YAKE

MIAKA1000 ELIYA
KONGOZI WA MAKUHANI KIZAZI CHA NNE.

UFUNGUO
=     Tunamshukuru MUNGU kwa ajili ya siku ya saba siku ya mafuta 7 ya ukamilifu ya vizazi vyote na majira na nyakati. Alichokisimamisha MUNGU ni kufanikiwa, kubarikiwa na kuogezeka milele.
=     Siku ya ukamilifu ya ile mbegu ya rohoni ikikamilika kwetu kwa ukamilifu.
=     Mbegu zingine zote za mwili, mtu na mwanadamu, kabila dini na madhehebu MUNGU amezifuta kamwe hazitasimama tena.
=     Tunamshukuru MUNGU kwa kukamilisha mbegu ya rohoni
=     Tunamshukuru MUNGU siku ya leo yale majeshi yote ya Dan.2:34.
+     Utawala wa dhahabu umefutwa.
+     Utawala wa shaba umefutwa.
+     Utawala wa fedha umeondolea.
+     Utawala wa udongo na chuma umefutwa.
=     Mambo mabaya yote yaliyokuwa yametengenezwa na sanamu na falme zote zilizokuwa zimetengenezwa na sanamu zimefutwa.

Dani.2:29-34
+     Nyumba ya Wakaldayo imevunjwa.
+     Nyumba ya Wayunani imevunjwa.
+     Nyumba  ya Warumi imevunjwa.
+     Nyumba ya Dini na Madhehebu imevunjwa kabisa.
=     Majengo yote ya Wakaldayo MUNGU ameharibu .
+     Majengo ya Wayunani
+     Majengo yote ya dini na dhehebu
=     Na hayo ndio yalisimama rohoni yalikuwa yakipinga nyumba ya MUNGU isisimame rohoni. Mpaka falme zote zimevunjwa ndipo nyumba ya MUNGU imesimama.

MSINGI
Jana MUNGU kwa kutumia kinywa cha Kiongozi wa Makuhani  kizazi cha nne.
Limejengwa agano la ufahamu wa kuishi rohoni. Kulikuwa na namna ya ugumu kwa wakamilifu kuishi rohoni bila ugumu huu kuondolewa nyumba ya MUNGU isingejengwa.

Kumbe kulikuwa na kisiki kilichokuwa rohoni kilisababisha ugumu.
Kilikuwa kinazuia jengo lisiweze kusimama na kila jengo likitaka kusimama kisiki kilikuwa kinazuia.
Dan.4:4-
Kisiki hiki ni:
Akapaza sauti yake……………
Sasa hiki ni kisiki kilikuwa kimebakia kikimzuia mkamilifu kukamilika yeye kama jengo.

Ayub.14:7
Kwa yapo…..
Kama kuna shida ndani yako kuna kisiki.
Kama kulikuwa na chembe chembe cha kisiki ndani yako jengo haliwezi kujengwa.

Kama kulikuwa na kisiki cha dini na dhehebu hicho kisiki kitachipua na kuota tena na kuwa jengo tena.

Tunamshukuru MUNGU nyumba mbayo ilikuwa tayari imebolewa nyumba ya dini na dhehebu ni tabia za asili, bonde la uvuli wa mauti lakini Nabii Eliya alilivunja na kuteketeza kabisa na halitachipua kabisa jana kisiki kiling’olewa na kuondelewa kabisa.

Dan.2:34-35
Kulikuwa na sanamu…
Dhahabu -kichwa Nebukadreza-Wakaldayo.
Fedha- kifua-Myunani.
Shaba -kiuno cha sanamu hiyo ambaye ni Mrumi.
Udongo na chuma ikimaanisha dini na madhehebu.
Nashukuru MUNGU kwa kuwa hiyo ilikuwa imesimama rohoni na kuzuia jengo lisisimame lakini jana MUNGU ameibomoa kabisa na haitasimama kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.
Wengi walikuwa hawajajua jengo maana yake nini
Jengo ni kama vile watoto wa Iran hawashawishiwi kuvaa hijabu.

Wakamilifu hata siku moja hawawezi kumwaga damu kwa kuwaonyesha kuwa wao wana MUNGU.

Waislamu wakiwa kwenye ndege angani hawaogopi kusali na kuwaonyesha jengo la nyumba yao imesimama.

Ifikifika muda wakutoa zaka zao wakati wa mwezi wa ramadhani wanagawa tena anatoa kwa ukamilifu bila kuogopa yeyote.

Kila alichokuwa anafanya Eliya ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI ilikuwa kwa unabii lakini sasa hivi linaonekana wazi wazi.

+     Majengo ya magonjwa yamefutwa.
+     Majengo ya mila na desturi yamefutwa.

Majengo yote yaliyojikita kwenye nafsi na kwenye roho hayo majengo yanatakiwa kubomolewa kwa Damu ya Haki kweli na Hukumu

+     Jengo lililokuwa ndani ya Petro limefutwa.
+     Jengo la ukabila limefutwa.
+     Jengo la mila na desturi limefutwa.
+     Jengo la tabia ya asili limefutwa.
+     Jengo la Dini ya Kiyahudi lilikuwa ndani ya Petro limefutwa.
+     Mpaka MUNGU akamwambia nilichokitaka usikiite najisi.
+     Mpaka MUNGU alisema naye mara tatu.
+     Tunamshukuru MUNGU jana jengo lilitolewa nafsi yake.
Kuanzia sasa hivi tutafanana ndani na nje kwa
·        Mfumo
·        Utendaji
·        Kwa kazi

Kuanzia sasa hivi dini na madhehebu, mila na desturi zitakufa kwa sababu jengo ni la rohoni sio la mwilini.

+     Nyumba sio matofali
+     Tunaposema nyumba Hagai.2:9 sio nyumba nyenye mabati

Sasa tunapakwa mafuta ya jengo moja rohoni na majengo mengine yote yanaondoka.

Baba yetu wa rohoni alitupa shamba na hatukupanda mbegu rohoni lakini leo tunapanda mbegu rohoni.
·        Siku ya kwanza nuru
·        Siku ya pili anga
·        Siku ya tatu maji
·        Siku ya nne mianga miwili mikubwa
·        Siku ya tano MUNGU aliumba nyangumi
·        Siku ya sita alichipusha miche
·        Siku ya saba alistarehe pande zote
·        MUNGU alijenga kwa siku saba.
·        Hata wewe utajenga kwa siku saba.
·        Na sisi msingi umeshakamilishwa nyumba inakamilika.

Leo tunasimamisha nyumba moja peke yake rohoni na tunafanana kuwa wamoja.

Hutapata shida tena kuja ibada ya majibu
na tutaongezeka sasa.

Hutapata shida tena kutoa fungu la MUNGU au shukrani
maana tunayo mbegu njema rohoni na kila mmoja atapata mafanikio kwa sababu ya mbegu njema rohoni.
·        Hutaogopa kuvaa vazi jeupe.
·        Hatutasimama kwa sababu ya katiba ya Kanisa

Kuanzia sasa zile mila desturi tulizokuwa tunaona hayo yote ni majengo sasa yanaanguka.
·        Amani itabaki Kanisani.
·        Ushindi utabaki Kanisani.

Wote mnaofanya kwenye sekta mtapanda mbegu ya amani kwa taifa. Wasi wasi, mashaka, hofu na woga vyote vilivyokuwa mjini vitafutika moja kwa moja.

Mwa.31:22-38
Hata siku ya tatu Labani akaambiwa Yakobo amekimbia…
Kumekuwa na mchezo wa waovu wanakwenda barabarani wanasota ina maana wanachafua Kanisa.

+     Tusije tukaingia na vinyago vya Labani

Hii mbinu ambayo walikuwa wanatumia kujifichia tunafuta kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

1Kor.3:9-16
Maana sisi tuwafanyakazi…
·        Sisi ni shamba la MUNGU.
·        Sisi ni roho.

Leo unajengwa kuwa jengo la MUNGU na kila moja hatakuwa na matusi. Kila moja hatakuwa mwepesi wa kufyonza huwezi kukasirika kwa sababu jengo la MUNGU liko ndani yako. Na hakuna atakayepata uvivu kuja kwenye ibada ya majibu.

·        Mimi leo na kuwa ushuhuda wa jengo la rohoni.
Baba yetu wa rohoni alitupa shamba la rohoni lakini hatukupanda mbegu ya rohoni.
Tunamshukuru MUNGU kuwa wote watatujua hakuna atakaye vaa carwash, taulo anatembea hakuna atakaye kula mahindi barabarani wote tuna tabia moja. Kila wakikuona lugha, mwendo wako wanajua huyu ni wa Siloam na hakuna atakaye mkata mwingine.

Yer.50:19-20
Siku hiyo ikifika tutafuta dhambi, uovu hatutauwona.
Kila kitu kibaya kitatafutwa kwako hakitaonekana.
Kama vile walivyomtegea Daniel wakasema labda tumtegee kwa sheria ya MUNGU wake lakini hawakuweza.

+     Jengo lenye utukufu kuliko kizazi cha 1,2,3.
+     Kama kichwa wako hajaja hapa lazima aje.
+     Kanisa wako hajaja hapa lazima waje.
+     Watoto wako ambao hawajaja hapa lazima waje.
+     Hata huo ufalme unaokukataza usipige makofi haupo.
+     Lazima tumpende MUNGU kwa sababu anataka tufanane wote.
+     Kila mmoja atapenda awe kwenye hilo jengo.
+     Katika hili jengo siachwi.
+     Majengo ya kabila, lugha na jamaa yote nayabomoa.

Majengo ni mila, desturi, mazoea, tamaduni mbaya zote yalikuwa yanasonga jengo ya MUNGU.

Zile ndoto mbaya ulizokuwa unaota zilikuwa zinatokana na majengo hayo.

+     Yale majinamizi yalikuwa yanakuzonga yote yamebomolewa

TOBA
1.  MUNGU atusamehe kwa ajili ya Joshua, Elisha, Timotheo, Petro na Paulo hawakufanikiwa kujenga jengo juu ya msingi la kizazi 1,2,3 halikuwahi kuonekana lakini kizazi hiki cha nne lazima jengo lionekane.

2.  Toba ni kizazi cha tatu wametupasia sisi maana yake hujui ni Petro, Tito, Timotheo na Paulo wakati alisema ni mkuu wa wajenzi kizazi 1 Joshua, kizazi 2 Elisha lakini kizazi cha tatu hatujui ni nani. Warumi wanamtaka Petro, Waluteri wanamtaka Timotheo, Tito na Wapentekoste wanamtaka Paulo.

Mahali popote unaona aibu ya kushukuru kwenye ndege na hoteli haitakuwepo tena kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

MWANZO WA SOMO
1Kor.3:9
Jambo lile la kila mmoja la kufanana na mwingine halikuwahi kutokea Kanisani siku zote, hatujawahi kutembea na mbegu ya rohoni na matokeo yake tunatembea kwa taabu sana.

Hilo lilisababisha hata ukiwa kwenye sinagogi unasena niko kwenye jengo. Wewe ukisimama na msingi wa rohoni wanaona kama unajifagilia kwa sababu hawakuwahi kuwa na msingi wa rohoni. Hakuna atakayeshindwa kujenga tabia ya MUNGU kwenye famila yake.

Unaona upande wa pili wanajenga petrol station wanajenga msikiti kwa sababu walikuwa na mbegu ya rohoni. Na vitu vingi vya MUNGU viliibiwa kwa akina Isaka, Yakobo kwa sababu mbegu zilikuwa za mwili sio za rohoni.

Wakamilifu wakiwa ibadani wanashangilia lakini wakitoka nje wanauliza tulikuwa tunashangilia nini kwa sababu mbegu ya rohoni haikuwepo.

+     Leo tutapanda mbegu ya rohoni iote moja kwa moja.

Kila mmoja lazima aje ibadani hata kama atakaa kwa muda mfupi kwenye ibada ya majibu ili apande hiyo mbegu na kuondoka. Wale mabinti wakubwa nataka niwaone wakija kila siku ibada ya majibu na mbegu ya rohoni ili iweze kuota tusiibiwe tena

Hata wale walioweka tumbo hapa madhabahuni nataka niwaone wakija kila siku ibada ya majibu na mbegu ya rohoni ili iweze kuota tusiibiwe tena.

Kama unataka nyumba, kiwanda na shamba nataka mje kila siku ibada ya majibu na mbegu ya rohoni ili iweze kuota isiibiwe tena.

Upande mbegu ya nyumba kuanzia kiwanja msingi na jengo. Leo tuna siku saba zikiwa zimekamilika tunaanza kupanda hiyo mbegu. Kwa nini jengo halikuweza kujengeka kizazi 1,2,3? Sisi lazima tujenge kwa Damu ya Haki Kweli na Hukumu.

Kwa nini akina Paulo na Timotheo walishindwa?
1.  Walishindwa kutofautisha msingi na jengo
Msingi wa nyumba umeshika hili jengo
Wale ambao walijenga msingi na jengo na wale ambao walishindwa kutofautisha ilisababisha Joshua ashindwe kujenga jengo.

Jengo sio mabati bali ni tabia ya MUNGU ionekane ndani ya kusanyiko takatifu. Wakati wa Joshua taifa la Mungu lilikosea wakarudi Babeli. Wana wa Israel hawaolewi nje wala kuoa nje hawakuja waliyofanya Joshua na Musa huo ufalme umeanguka?

2.  Kushindwa kuelewa vizuri yule anayejenga jengo kama vile anayejenga msingi
Pia inakuwa sababu ya kushindwa kufanikiwa kujenga jengo
Mfano kila kitu MUNGU anachokileta kinapitia madhabahuni na anayejenga jengo anapitia madhabahuni kama hamkumwelewa maadui wanapata nafasi. Lazima kumwelewa anayejenga jengo kama anayejenga msingi hapo vitu vyetu tunapokea maana MUNGU anakaa kwenye ufahamu. kadri unavyomwelewa MUNGU na Kristo na anayekaa madhabahuni ndivyo unavyopokea haja ya moyo wako.

Kut.17:11-16
Mikono ya Musa ilipokuwa ina teremka chini Israel walikuwa wanapigwa kwa sababu mikono yake ilitakiwa ije juu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Yos.7:1-
Waliposhindwa kumwelewa Joshua walishindwa na sisi tunatakiwa kumwelewa anayesimama madhabahuni ambaye anajenga jengo kama vile aliyejenga msingi.

Katika hili MUNGU atupe neema ya kumwelewa MUNGU kila siku anayoongea tutasema ni Miaka1000 anasema. Tunataka MUNGU atupe neema kuwa jengo la MUNGU mwenyewe, lakini ni mpaka tumwelewe anayejenga jengo kama anayejenga msingi.

3.  Kufurahisha mwili
Ukisoma matendo yote hata Paulo, wanafunzi wa Yesu walikuwa wanakwenda vizuri. Baada ya Yesu kuhama kituo Wayahudi wakawashinda nguvu.

Pia aliwaambia hivi mnataka niwe Mkristo mila zote zije kanisani wakafurahisha mwili. Hapo ndipo walipoanza kusema bikira maria tuombee kwa mwanao. Timotheo na Tito alishindwa kwa sababu alilazimika kuwafurahisha Warumi. Sisi tuna neema kubwa kwa sababu Kristo amevunja kabisa mila na desturi.

Sisi hatutashindwa ndiyo maana tumepewa mbegu ya rohoni.
Waluteri walitaka kurudisha kanisa kutoka kwa Warumi lakini walishindwa, Wapentekoste waliokuja miaka 100 iliyopita hawakuweza. Kitendo cha Eliya kurudisha majira na nyakati ni ili tusije kutoka rohoni na kurudi mwilini lakini sisi tumeshinda.

4.  Ugumu wa kuishi rohoni
Hata sisi tulikuwa bado tunasumbuliwa lakini kuanzia leo ugumu huo hautatusumbua. Yaani unapata 10,000 unatoa elfu moja lakini ukipata milioni moja hatuwezi kutoa fungu la kumi.

Kumekuwa na ugumu wa kuishi rohoni kwa kuangalia mazingira. Anakuja ndugu yako saa ya kuja ibadani huji tena ibadani unazungumza naye huo ni ugumu wa kuishi rohoni leo lazima tushinde hapo ili jengo liweze kujengeka. Usione kama hawampendi MUNGU wa Eliya bali ni ugumu wa rohoni. Unafurahi lakini unaanza kusema alilosema Miaka1000 linawezekana kweli hilo linasababisha ugumu wa kuishi rohoni.
Kumekuwepo na ugumu wa kuishi rohoni lakini jana tulibomoa moja kwa moja. Wengi tuna watoto na wengi tumeolewa lakini nyumbani tunaweza sana kuweka ibada asubuhi na jioni. Tukiwa na ibada nyumbani MUNGU awafungue macho uone taa nyumbani kwa wakamilifu. Unapoacha kufanya ibada asubuhi na jioni usabababisha udhaifu.

Tumekuwa na tabia wengi tunakuja na vazi jeupe baadaye tunabadilisha na kuvaa vazi la rangi kwa sababu tunaogopa kuambiwa unasali Siloam huo ni ugumu labda kuna maswali watakuuliza utashindwa kujibu. Mfano waislamu ikifika ijumaa hawaogopi kuvaa vazi lao, ikifika saa saba wanafunga maduka yao mpaka warudi ndipo wawahudumie. Ikifika saa ya ibada hata kama unasonga ugali kama unakauka uache ukauke unatakiwa ufanye ibada.

Leo lazima tufike hapo wote tuwe na tabia moja kama ni saa mbili tuwe na ibada lazima iwe hivyo. Na wengine tunakurupuka tu hatufanyi ibada hata kwenye dala dala unatakiwa umwambie MUNGU leo nikienda kwenye ibada nataka hiki nataka hiki. Niliwaambia sauti ya agizo wao wanatakiwa kufanya ibada ili ijulikane, ule ugumu wa kuishi rohoni unafutwa moja kwa moja. Waliokuwa na hiyo mbegu walikimbia nayo wenye haki walikuwa wanaishi mwilini na waovu wanaishi rohoni.

Kuna tabia unaingia kwenye shukrani unaombea kitu ukimaliza huamini tena kama MUNGU atajibu huo ni ugumu wa kuishi rohoni. Wengi wanaofaidi vitu vya Siloam ni wale wanaokuja siku moja akitoa sadaka yake mara moja anafaidi kwa sababu wanaamini. Leo kuanzia sasa hivi kwa hii mbegu tunayopanda siku saba hatutakuwa tena na ugumu wa rohoni.

Pia mabinti msipate shida kuvaa vazi refu hiyo ndio mbegu ya rohoni. Hakuna atakayechumbiwa kwa kuvaa vazi fupi wala hutapendwa kwa kuwa kitovu chako kinaonekana. Imefika wakati tuwe na mavazi ya heshima, kijana hutapendwa kwa sababu ya mlegezo au chupi inaonekana lazima tufike wakati wa kuvaa mavazi ya kupendeza. Hutapendwa kwa kunyoa panki utapendeza ukinyoa kawaida.

Leo jengo la Bwana limesimama tabia ya MUNGU ionekane wote wajue hii ni Siloam. Taifa limetafuta vazi la taifa na wote wanasubiri waone vazi la taifa hapa. MUNGU amechagua taifa hili kwa sababu ya agizo liko katika taifa. Anayetaka kuharibu agizo Miaka1000 hana ushirika naye maana ametufundisha kuvaa mavazi marefu.

Tabia moja ukienda Elimu unakuta tabia hiyo hiyo, Patmo ukienda unakuta tabia hiyo hiyo, ukienda taifa lolote hilo ndio jengo la MUNGU kizazi cha nne. Hilo ndio jengo ambalo linajengwa kwa mbegu ya rohoni.
Tumeshapewa nchi nzuri la umilele lakini halijapewa mbegu. Na tunaingia kipindi cha pasaka na kila unachotamani utakipata kwa sababu ya hiyo mbegu.

Rum.8:2
5.  Sheria ya roho unatupa uzima

Sasa hivi ukienda kijiji na kuwaambia mila hii ni mabaya wataacha kwa sababu rohoni ilishabomoka. Ndiyo maana sasa hivi kila mmoja ni Kuhani. Jengo ambalo ni la taifa moja lugha moja, sura moja, vazi moja, utaratibu moja, katika kazi moja, huduma moja na familia moja.



No comments:

Post a Comment